Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AHMED ALLY SALUM AOMBA KURUDI TENA UBUNGE JIMBO LA SOLWA


Mbunge wa Jimbo la Solwa anayemaliza muda wake, Mhe. Ahmed Ally Salum, ameibuka tena kwa kishindo akiomba ridhaa ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumchagua kwa kura ya “NDIYO” ili aendelee kulitumikia jimbo hilo kwa awamu nyingine.

Katika kampeni zake za awali, Ahmed Salum amesisitiza kuwa dhamira yake kuu ni kuendeleza kasi ya maendeleo kwa vitendo kupitia kaulimbiu yake ya “Kazi na Utu, Tunasonga Mbele.

Ndugu wanachama, safari yetu bado haijakamilika. Tumefanikisha miradi mikubwa ya miundombinu, elimu, maji, afya na mambo kadha wa kadha. Sasa ni wakati wa kuongeza nguvu zaidi. Naomba kura ya NDIYO ili tuzidi kusonga mbele kwa maendeleo ya Solwa,” amesema kwa hamasa.

Ahmed Ally Salum amejipambanua kama kiongozi makini, mchapakazi na mwenye rekodi ya utekelezaji wa miradi inayogusa maisha ya wananchi.

 Ameahidi kuendeleza miradi ya ujenzi wa barabara za vijijini, kuboresha huduma za afya na kuimarisha uchumi wa wananchi.

🗳 "Oktoba tunatiki! Kura ya NDIYO kwa Ahmed Ally Salum ni kura ya maendeleo kwa Solwa."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com