Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TAASISI YA MTETEZI WA MAMA YAHAMASISHA KULINDWA KWA HAKI ZA KIJINSIA CHALINZE

Mwenyekiti wa Taasisi ,Chalinze Bw. Godfrey Mtegetwa akifungua kikao
Katibu wa hamasa Taifa, Bw. Rimfried Chowalo
Mwenyekiti wa Taasisi mkoa wa Pwani, Habiba Tingisah
Afisa TEHAMA wa Taasisi ya mtetezi wa mama Taifa, Bw. Edward Mtemi akizungumza na wadau wa taasisi hiyo.

NA ELISANTE KINDULU,CHALINZE

TAASISI ya Mtetezi wa Mama imewataka wanachama wake na wadau wengine wa haki, kulinda haki za kijinsia katika jamii zao.

Hayo yalisemwa na Afisa teknolojia ya Habari na mawasiliano kutoka Taasisi ya mtetezi wa mama Taifa Bw. Edward Mtemi alipokuwa akizungumza na wanachama wa taasisi hiyo wa Halmashauri ya Chalinze mjini hapa jana.

Bw. Mtemi alisema lengo la taasisi hiyo ni kuwakomboa wanamke, watoto na wazee ambao ndilo kundi lililokuwa kwenye changamoto kubwa ya kutafuta haki katika jamii.

Afisa TEHAMA huyo aliwataka wanachama hao kutoa elimu ya haki ya kijinsia bila woga ili kulikomboa kundi hilo maalumu kwenye jamii.

"Walindeni wazee ,watoto na akina mama. Mnajua Kuna lindi kubwa la ubakaji, vipigo kwa wanawake na wazee wasiojiweza kufanyishwa kazi kinyume na uwezo wao kupitia miradi mbalimbali ya kujitolea kwenye jamii ilhali wengine wamo kwenye mfumo wa kusaidiwa na taasisi mbalimbali ikiwemo TASAF",amesema.

Aidha kiongozi huyo amewasisitiza wanachama hao kuwaunganisha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kuhakikisha wanajiunga katika vikundi vya ujasiliamali na kupata fursa ya kuinua uchumi kupitia mikopo katika taasisi za fedha pamoja na ile inayotolewa na halmashauri za wilaya nchini.

Afisa TEHAMA huyo amesema tasisi hiyo inaunga mkono juhudi za maendeleo chini ya uongozi wa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na taasisi inatarajia kushiriki uzinduzi wa kampeni za chama zinazotarajiwa kufanyika tarehe 28 mwezi huu katika Viwanja vya Tanganyika packers jijini Dar es Salaam, kwani taasisi yao imebahatika kupata kibali hicho cha kushiriki uzinduzi huo.

"Katika uzinduzi, tupo pamoja kuunga mkono serikali ya awamu ya sita. Tukimaliza hili tunarudi kwenye majukumu yetu ya kawaida ya kitasisi ya kumkomboa mama na mtoto",amesema.

Viongozi wengine walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Katibu hamasa Taifa Bw. Ramfriel Chowalo, Afisa Uhusiano, Bw. Twaha Twahibu, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo mkoa wa Pwani Bi. Habiba Tingisah, Afisa Habari wa Taasisi mkoa wa Pwani Bi. Mwanaasha Omari na Afisa mipango Bi. Salome Sidoyeka.

Akifungua kikao hicho, Mwenyekiti wa taasisi ya mama wa Halmashauri ya Chalinze Bw. Godfrey Mtegeta amesema Hamashauri ya Chalinze ina kata 15. Jukumu lililopo mbele yao ni kuhakikisha taasisi inapata wanachama katika kata zote za halmashauri hiyo.

Kikao hicho kiliwashirikisha viongozi na baadhi ya wanachama wa taasisi hiyo wa halmashauri ya Chalinze.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com