Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MPINA AZUIWA KUINGIA OFISI ZA INEC KUREJESHA FOMU YA URAIS


Mgombea wa Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina akionyesha begi la fomu akiwa amesimama nje baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya ofisi za INEC kurejesha fomi hiyo ya kuomba ridhaa ya kuwania nafasi hiyo.

**
MGOMBEA wa Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Luhaga Mpina amezuiwa na askari kuingia katika ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kwa ajili ya kurejesha fomu za kuwania nafasi hiyo.

Mpina amewasili majira ya saa 6:40 mchana akiwa na wanachama wake ambao wote walizuiwa kuingia ndani ya geti la Tume huku wanachama wake wakitaka kujua sababu ni nini ya kuzuiliwa.

Kutokana na hilo muda mchache walisomewa vyama vinavyotakiwa kurejesha fomu ni 17 ambapo ACT imetolewa kwenye orodha ya vyama hivyo.

Hata hivyo walitakiwa kukaa pembeni ili wale waliowazuia wapate majibu kutoka INEC huku wakimwambia Mpina atulie ndani ya gari huku akisubiri majibu kama ataingia Tume au atazuiliwa.

Wanachama hao walitii kile walichoambiwa na kusogea mita chache kutoka geti hilo la INEC ambapo nje ya geti hilo kulikuwa na ulinzi wa kutosha ndani na nje.

Kadhalika wanachama hao walionyesha kufuata maelekezo waliopewa na askari waliokuwa getini.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com