
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) leo imetangaza rasmi majina ya wagombea wa ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa Majimbo ya Shinyanga Vijijini, na sasa ni wazi wanaingia vitani kuchuana na wagombea wa vyama vingine katika uchaguzi mkuu ujao.
Ahmed Ally Salum ameteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika Jimbo la Solwa na
Azza Hillal Hamad atagombea ubunge wa Jimbo la Itwangi.
Wagombea hao wameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi bega kwa bega ili kuendeleza miradi ya maendeleo, hususan katika sekta za elimu, afya, maji na miundombinu.
Wanachama na viongozi wa CCM katika maeneo husika wamepokea taarifa hii kwa furaha kubwa na mshikamano, wakiahidi kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni na hatimaye katika upigaji kura.




Social Plugin