
Ni rasmi sasa! Ahmed Ally Salum amerudi tena kwa kishindo katika siasa za Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga baada ya kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi kuipeperusha bendera ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Hii ni habari ambayo imepokewa kwa hisia tofauti: upande mmoja kuna furaha na shangwe kwa wafuasi wake wanaoamini yeye ndiye chaguo sahihi la Solwa, upande mwingine kuna minong’ono ya kisiasa kwamba “Game imeisha mapema” kutokana na jina lake kukubalika kwa muda mrefu katika jimbo hilo.
Ahmed Ally Salum si jina jipya. Ni kiongozi aliyeacha alama katika siasa za Shinyanga na mara kadhaa ameonesha kwamba ana uwezo wa kupenya kwenye changamoto ngumu za kisiasa.
Kwa uteuzi huu, ujumbe kwa wapinzani ni wazi: Solwa siyo maabara ya majaribio ya kisiasa – ni ngome ya Ahmed Ally Salum na CCM.
Wanaomfuatilia kwa karibu wanasema safari yake ya kisiasa imekuwa na milima na mabonde, lakini sasa ameibuka tena akiwa na kadi moja ya ushindi mkononi uteuzi wa CCM.
Kwa upande wa wananchi, matarajio ni makubwa. Wanatarajia kusikia mipango yake ya kuimarisha huduma za jamii, miradi ya maendeleo na kupigania maslahi ya Solwa bungeni.
Hata hivyo kwa macho ya wachambuzi wa siasa, uteuzi huu ni zaidi ya jina ni signal ya CCM kwamba Solwa bado inahitaji “mchezaji mwenye uzoefu wa kisiasa” kuiongoza safari ya maendeleo.
Social Plugin