Mgombea Ubunge, Ahmed Ally Salum amerudisha rasmi fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), hatua inayojidhihirisha kama mwanzo wa safari ya kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Tukio hilo limefanyika Leo tarehe 27 Agosti 2025 katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Viongozi wa chama waliomsindikiza Salum wamempongeza kwa hatua hiyo, wakiashiria mshikamano na kuahidi kumpa ushirikiano wa karibu katika kampeni zake, kwa lengo la kuhakikisha ushindi wa kishindo katika jimbo hilo.
“Hatua hii ni ishara wazi ya mshikamano wa ndani wa CCM na maandalizi makini ya ushindi wa kishindo,” amesema mmoja wa viongozi wa chama aliyehudhuria tukio.








Social Plugin