
Familia ya Bwana Jabili Athumani, mkazi wa Mtaa wa Mshikamano, Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga, inakabiliwa na changamoto kubwa baada ya binti yao, Swaumu Jabili (22), kulala kitandani kwa miaka 8 mfululizo kufuatia ugonjwa wa kupooza upande mmoja wa mwili alioupata akiwa darasa la saba mwaka 2017.
Akizungumza na Malunde 1 Blog, Mama Swaumu, Bi. Aza Juma, amesema binti yake alianza kuonesha dalili za matatizo ya kiafya akiwa na umri wa miezi minane tu, lakini baadaye alipata nafuu na kuweza kuhudhuria shule kama kawaida. akiwa darasa la saba mwaka 2017, hali hiyo ilirudi kwa kasi na kumfanya kupooza kabisa na kushindwa kutembea.
Nguzo pekee waliokuwa wakitegemea kwaajili ya kupata mkate wa kila siku kutoka kwa baba wa familia hiyo Jabili Athumani nayo imeanguka baada ya tarehe 04/04/2025 kupata ajali ya pikipiki wakati akiwa kwenye shughuli za kujipatia riziki kwa ajili ya familia yake ajali iliyopelekea kukaa ndani kwa muda wa miezi 4 sasa.
Mzee Jabili anasema kuwa kabla ya kupata ajali kama kiongozi wa familia alijaribu kutafuta matibabu kwenye hospitali mbalimbali lakini majibu waliyopewa na madaktari kutoka hospitali ya kanda Bugando jijini Mwanza ni kuwa upande mmoja wa ubongo binti yake umeharibika.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalonga, Victor Ocheng’i, amesema baadhi ya majirani na wasamaria wema wamekuwa wakijitahidi kusaidia familia hiyo kadri wawezavyo, lakini bado mahitaji ni mengi, hivyo ameziomba taasisi, mashirika na watu binafsi kujitokeza kuwasaidia.
Familia ya Mzee Jabili kwa sasa inaomba msaada wa fedha kwa ajili ya dawa za kupunguza maumivu na zaidi wanahitaji kiti mwendo kitakachomuwezesha binti yao kupata urahisi wa kuhudumiwa na kujimudu katika shughuli za kila siku.
KWA YEYOTE ATAKAYEGUSWA KUISAIDIA FAMILIA HII ANAWEZA KUWASILIANA AU KUTUMA MCHANGO WAKE KWA NAMBA YA SIMU YA FAMILIA (0754 630 284) - JABILI ATHUMANI SWALEHE (Baba wa Familia).
Mama wa familia hiyo Bi. Aza Juma akizungumza na Malunde 1 Blog.
Baba wa familia hiyo Jabili Athumani akizungumza na Malunde 1 Blog.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kalonga, Victor Ocheng’i akizungumza na Malunde 1 Blog.
Social Plugin