Jengo la Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga
Na Sumai Salum – Kishapu
"TAKUKURU kwa kushirikiana na Jamii, ngome ya Haki na maadili ya maendeleo ya kweli"
Rushwa haimalizwi kwa maneno, bali kwa vitendo na vitendo hivyo vinaanzia kwa mtu mmoja mmoja kusema "Hapana Rushwa!" iwe ni shuleni,Vyuoni, ofisini,sokoni, au kwenye Uchaguzi.
Ni wakati wa Wananchi, Viongozi, na Taasisi zote kushikamana katika mapambano haya. Rushwa haiwezi kumalizwa na TAKUKURU peke yake, bali kwa kushirikiana, kutenda kwa maadili ya pamoja na kwa kuamini kwamba Tanzania mpya inawezekana.
Katika harakati za kuijenga Tanzania yenye uwazi, usawa na maendeleo endelevu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imeendelea kuwa mhimili wa matumaini kwa wananchi. Kwa zaidi ya miongo miwili, TAKUKURU imekuwa mstari wa mbele katika kupambana na adui mkubwa wa maendeleo Rushwa.
Lakini je, Jamii inaelewa kwa undani umuhimu wa taasisi hii katika maisha yao ya kila siku?
Katika jamii yoyote yenye utawala wa sheria, haki na usawa ni msingi wa misingi bora kwani Rushwa huvunja misingi hiyo kwa kutoa upendeleo, kuua haki, na kuzuia fursa kwa watu wenye uwezo wa kweli.
TAKUKURU inapojikita kuzuia vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma za jamii kama Afya, Elimu, Ajira na Zabuni za Maendeleo, inawalinda wananchi wasionewe au kukosa huduma kwa sababu hawakuwa na "cha juu".
Katika uzinduzi wa jengo jipya la TAKUKURU Kishapu Mkoani Shinyanga mnamo June 25,2025 wananchi walitoa wito wa kuongeza elimu ya kuzuia rushwa, jambo linaloonyesha kiu ya haki na wananchi wanaelewa kuwa TAKUKURU si adui wa watu bali ni mlinzi wao.
Elimu ya Kuzuia Rushwa ni Nguzo Muhimu ya Mabadiliko ya Tabia
TAKUKURU haipaswi kuonekana kama chombo cha kukamata watoaji na wapokeaji Rushwa pekee kwani kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bw.Crispin Chalamila wakati akizindua jengo hilo alisema "jukumu kubwa la Taasisi hiyo ni Kuzuia Rushwa kabla haijafanyika". Na hili linawezekana kwa elimu.
Kutoa elimu kwa Jamii Mashuleni, kwenye Vikundi vya Wanawake, katika Mitandao ya Vijana, hadi kwa viongozi wa Vijiji ni njia muhimu ya kujenga kizazi kinachochukia Rushwa, badala ya kuiona kama njia ya mkato kufanikisha mambo.
Uelewa wa wananchi kuhusu aina za Rushwa (ikijumuisha Rushwa ya ngono, kisiasa, au ya ofisini) unapaswa kuwa wa kina ili waepuke na wapinge vitendo hivyo kwa ujasiri.
TAKUKURU ni Dira ya Maadili ya Taifa
Jamii isiyojali maadili hujenga msingi wa uharibifu wa baadaye. Rushwa huambatana na uongo, udanganyifu, uzembe, ubinafsi na mwisho wake ni kuvunjika kwa maadili ya kazi na uongozi.
Kwa kuimarisha TAKUKURU, serikali inajenga chombo cha kuhimiza nidhamu serikalini na sekta binafsi kwani Watumishi wa umma na binafsi wanapojua kuwa kuna macho yanayowatazama, wanajikita kwenye wajibu na si ubinafsi hii hufanikisha utendaji kazi uliobora na unaojali wananchi.
Wananchi wana wajibu wa kushiriki kwenye mapambano dhidi ya Rushwa kwa kutoa taarifa wanapoona viashiria au vitendo vya Rushwa na hili linawezekana iwapo TAKUKURU itakuwa karibu na watu, iwe rahisi kufikika, na iwe na mazingira rafiki ya kutoa taarifa kwa siri.
Jengo jipya la TAKUKURU Kishapu limeboreshwa kwa kuzingatia usiri wa utoaji wa taarifa ikiwa ni hatua muhimu ya kuondoa hofu na kujenga imani ya wananchi kwa Taasisi hiyo.
Rushwa kwenye chaguzi ni tishio kubwa kwa mustakabali wa maendeleo ya jamii husika na taifa kwa ujumla Mgombea anayehonga ili achaguliwe hawezi kuwa kiongozi mwenye dhamira ya kweli ya kuhudumia wananchi,Kwa hili,TAKUKURU ina jukumu kubwa la kuelimisha wananchi kutambua athari za kupokea Rushwa ya kisiasa.
Kama alivyosema Mkurugenzi Mkuu Chalamila, “Kukubali Rushwa kutoka kwa mgombea ni sawa na kukataa maendeleo yako mwenyewe.” Jamii ikielimika kuhusu hili, inaweza kuibuka na viongozi safi, wanaowajibika kwa wananchi na si kwa matamanio yao.
Umuhimu wa TAKUKURU hauwezi kupuuzwa ni mlinzi wa maadili, mtetezi wa haki, msukumo wa maendeleo na daraja kati ya wananchi na serikali yenye uwajibikaji.
Amos Masunga mkazi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga anatoa wito kwa TAKUKURU kutoka maofisini na kuwa karibu zaidi na jamii kwa kutoa elimu ya kupambana na Rushwa, hasa kwa makundi yaliyo hatarini kama WANAWAKE na VIJANA.

Mkazi wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Amos Masunga
Veronica Mussa Mkazi mwingine wa Wilaya hiyo amesema TAKUKURU inapaswa iwe macho kwa wagombea wanaotumia mbinu za kugawa fedha, khanga na vipande vya vitenge kwa wananchi kwa lengo la kuwashawishi ili wawapigie kura.
Uwepo wa jengo zuri la Taasisi hiyo ni hatua ya mwanzo, lakini mafanikio ya vita dhidi ya Rushwa yanahitaji mikakati shirikishi elimu, uwazi, na upatikanaji rahisi wa taarifa kwa wananchi wote.
Katika hotuba yake, Bw. Chalamila alisisitiza kuwa jengo hili ni sehemu ya mpango mpana wa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha Taasisi muhimu za uwajibikaji.

Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Bw. Chrispin Francis Chalamila
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, bajeti ya TAKUKURU imeongezeka kutoka Tsh. bilioni 1.5 mwaka wa fedha 2021/22 hadi Tsh. bilioni 6.0 mwaka wa fedha 2025/26, ikiwa ni uthibitisho wa dhamira ya kweli ya kupambana na Rushwa nchini pamoja na ujenzi wa majengo mapya, ukarabati wa majengo ya zamani, na uboreshaji wa mazingira ya ofisi.
Viongozi Watoa Ujumbe wa Kuleta Mabadiliko
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala,Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo, ametoa msisitizo kwa TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kwa haki na uadilifu, akisema taasisi hiyo imekuwa kiini cha matumaini kwa wananchi wanaotamani kuona nidhamu na uwajibikaji serikalini.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Utawala,Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Boniphace Butondo
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Peter Masindi, alitoa changamoto kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya Rushwa hasa wakati huu kuelekea uchaguzi mkuu.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi
Kazi ya kuzuia na kupambana na Rushwa ni ya pamoja kama kauli mbiu ya TAKUKURU isemavyo"KUZUIA RUSHWA NI JUKUMU LAKO NA LANGU TUTIMIZE WAJIBU WETU".
Kauli hii ni mwanga unaotuonyesha kuwa mapambano dhidi ya Rushwa hayatapaswa kuishia kwenye ofisi pekee bali pia katika maamuzi ya wananchi, hasa kwenye sanduku la kura hii ina maana kuwa elimu ya Rushwa inapaswa kulenga pia kuelewa maana ya ‘Rushwa ya kisiasa’ ambayo ubadili mustakabali wa maendeleo ya maeneo mengi nchini.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Shinyanga Donisian Kessy

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Atuganile Stephen

Social Plugin