Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu wa Maveteran kutokea Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi Julai 12,2025 kwenye viwanja vya mpira Shule ya Msingi Buduhe Wilayani humo
Na Sumai Salum – Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi amewapongeza wachezaji wa timu za maveterani kutoka Kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi kwa kuendeleza michezo kama njia ya kuimarisha afya, mshikamano na maendeleo ya kijamii.
Akizungumza Julai 12, 2025 katika uzinduzi wa mashindano ya maveterani yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe Wilayani humo, Masindi amewataka wachezaji na wadau wa michezo kutumia fursa hiyo kujenga mahusiano chanya, kujitangaza kibiashara na kuimarisha mshikamano .
"Michezo ni afya, michezo ni biashara, na michezo ni mahusiano. Huu ni wakati wa kutambua kwamba kukutana na watu ni fursa. Maendeleo ya binadamu yamejengwa juu ya misingi minne ikiwemo kumjua Mungu, kuwa karibu na watu, kujali muda na kuheshimu matumizi ya fedha,” amesema Masindi.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa amani na utulivu katika mashindano hayo, akiwataka wachezaji wote kuzingatia maadili ya michezo kwa kucheza kwa nidhamu na kuonyesha mshikamano na upendo wa hali ya juu.
“Rais wetu anapenda michezo, amani na utulivu hivyo mkiwa Kishapu, hakikisheni kuwa mnaonesha utulivu kwa vitendo," ameongeza Masindi.
Mashindano hayo yaliyohusisha timu za Kishapu,Kahama,Biashara,Msalala,Simiyu Dazo,Musoma,Shinyanga pamoja na Shy Town huku yakitarajiwa kufanyika kwa siku mbili kwa lengo la kuimarisha michezo ya wazee, kukuza vipaji na kutoa burudani kwa jamii.

Mashindano hayo yameandaliwa na Kishapu Veteran na kudhaminiwa na kampuni ya Zamseed, wauzaji na wasambazaji wa mbegu bora za kilimo hapa nchini huku yakihimiza kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba 2025,kataa Rushwa na pinga ukatili wa jinsia.
Mwenyekiti wa Kishapu Veterani ya Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sostenes Amas akizungumza kwenye uzinduzi wa mashindano ya mpira wa miguu yaliohusisha timu za Veterani kutoka kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi yaliyozinduliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi katika viwanja vya mpira Shule ya Msingi Buduhe Julai 12,2025

Social Plugin