Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALPHITONE MICHAEL BUSHI ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SOLWA


Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog

Alphitone Michael Bushi, aliyewahi kuwa dereva wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga katika Kitengo cha Afya, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge wa Jimbo la Solwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.

Alphitone Michael Bushi amechukua fomu hiyo leo Shinyanga, Julai 2, 2025 katika ofisis za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga vijijini.

Bushi ambaye amehudumu kwa miaka kadhaa kama mtumishi wa umma katika sekta ya afya, amesema amejifunza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa kawaida, hususan katika maeneo ya pembezoni, na hivyo kupata motisha ya kuingia katika siasa ili kusaidia kuleta mabadiliko chanya.

Akizungumza na wanahabari muda mfupi baada ya kutangaza nia hiyo, Bushi amesema azma yake ni kusimamia maendeleo ya wananchi wa Solwa kwa dhati, kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji, kata na halmashauri katika kubuni na kusimamia miradi ya kimaendeleo, hasa katika sekta ya afya, elimu, maji na kilimo.

Aidha, amewataka wanachama wa CCM katika Jimbo la Solwa kumpa nafasi hiyo ya kupeperusha bendera ya chama, akiahidi kuwa atakuwa mzalendo, mfuatiliaji wa maendeleo, na daraja kati ya wananchi na serikali. 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com