Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NYAMBARI NYANGWINE KUVAANA NA MWITA WAITARA UBUNGE TARIME VIJIJINI!

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempitisha Nyambari Chacha Nyangwine kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Tarime Vijijini, mkoani Mara katika mchakato wa ndani ya chama.

Uamuzi huo umetolewa baada ya kikao maalum cha Kamati Kuu kupitia na kujadili majina ya wanachama waliowasilisha nia ya kugombea ubunge katika mchakato wa ndani ya chama hicho tawala.

Kwa kupitishwa kwake, Nyambari atachuana katika kura za maoni dhidi ya makada wengine waliojitokeza kutaka kupeperusha bendera ya CCM jimboni humo, wakiwemo Mwita Mwikwabe Waitara (Mbunge aliyemaliza muda wake), Simon Kemor Chacha, Deodatus Waikama, na Edward Mgelea Machage.

Jimbo la Tarime Vijijini ni miongoni mwa majimbo yenye ushindani mkali katika siasa za Mkoa wa Mara, na mchuano wa ndani ya CCM mwaka huu unaonekana kuvuta hisia kali kutokana na uzito wa majina yaliyotajwa.

Kwa sasa, macho na masikio ya wanachama wa CCM na wananchi wa Tarime Vijijini yanaelekezwa kwenye hatua inayofuata ya kura za maoni, itakayotoa mwanga wa nani atakuwa mgombea rasmi wa chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com