
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Modester Machiya (Kulia) akimkabidhi Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Isoso Madam Jenipher Mushi (kushoto) bokisi la taulo za kike katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yariyoratibiwa na Kituo hicho Juni 16,2025.Picha na Sumai Salum
Na Sumai Salum-Kishapu
Kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Kinachoshirikiana na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP kimeadhimisha Siku ya mtoto wa Afrika kwa kutoa elimu ya masuala ya ukatili na kugawa taulo za kike katika Shule ya Sekondari Isoso Wilayani humo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo yaliyofanyika Juni 16,2025 Mwenyekiti wa Kituo hicho Modester Machiya amewakumbusha wanafunzi hao wa Kidato cha pili na Nne umuhimu wa kutambua kwa undani masuala yote ya ukatili na namna ya kuweza kuepukana nayo.
"Nyinyi sasa sio watoto wa kiasi cha kutojua ukatili wa aina zote na jinsi gani ya kuepukana nao, muwapo majumbani,mitaani na hata shuleni mnapaswa kujua mkifanyiwa ukatili wa aina yeyote ni nani mmuone ili aweze kuwasaidia kwani jukumu la kupinga vitendo hivyo kwenye jamii yote ni letu sote",amesema Machiya.
Kwa upande wake Katibu wa Kituo hicho Robert Majebele ameelezea umuhimu wa kukumbuka siku hiyo akiongezea kuwa kufuatia kumbukizi ya maadhimisho hayo kwa wanafunzi yafanyike chachu ya kuielimisha jamii na familia zao kuhusu madhara yatokanayo na ukatili yakilenga kupatikana kwa haki za mtoto.
Mwelimishaji wa mada ya haki za mtoto Getrude Boniphace Yahula amesema mtoto ana haki ya kupata elimu,chakula bira,kutobaguliwa,kusikilizwa,afya na haki ya kulindwa na ukatili wa kijinsia aina zote.
Mtoa mada ya pili kuhusu aina za ukatili Sophia George ameelezea aina mbalimbali za ukatili ikiwemo ukatili wa Kimwili,kielimu,Kiafya,kiuchumi na kisaikolojia.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamepongeza kwa maarifa waliyoongezewa na wamekiri kuwepo kwa ukatili wa kimwili na saikolojia kwa baadhi ya shule unaopelekea wanafunzi kutofanya vizuri darasani na kuwaomba Waratibu elimu Kata kuimarisha mahusiano mazuri kati ya waalimu na wanafunzi.
Mwakilishi wa Mkuu wa shule hiyo Madam. Jenipher Mushi amekipongeza kituo hicho kwa kutoa muda na Mali zao na kuwakumbuka wanafunzi hao wanaotoka maeneo tofauti ya Wilaya ya Kishapu na kuwataka wanafunzi yote waliyofundishwa kuhusu kuepukana na ukatili wanakuwa mabalozi wazuri kwenye jamii.
Maadhimisho hayo yenye lengo la kuhamasisha upatikanaji haki za mtoto huku Kituo hicho kikiungana na Taifa na mataifa mengine Barani Afrika kukumbuka vifo vya watoto 2000 wa Soweto Afrika ya Kusini walioandamana na kupinga ubaguzi wa elimu kwa serikali ya Makabulu Juni 16, 1976 yameambatana na kauli mbiu isemayo "Haki za mtoto tulipotoka, tulipo na tuendako".

Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Robert Majebele akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili na nne Katika Shule ya Sekondari Isoso kuhusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho wa siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na kituo hicho wakishirikaina na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Juni 16,2025


Mjumbe wa Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga George Bugali akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili na nne Katika Shule ya Sekondari Isoso kuhusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho wa siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na kituo hicho wakishirikaina na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Juni 16,2025






Mtoa mada ya Haki ya Mtoto kutoka Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Getrude Boniphace Yahula akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili na nne Katika Shule ya Sekondari Isoso kuhusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho wa siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na kituo hicho wakishirikaina na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Juni 16,2025

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Isoso Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Jilala Ntemi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu kwa kutoa elimu na ugawaji wa taulo za kike Juni 16,2025

Mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Isoso Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joyce Amos akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu kwa kutoa elimu na ugawaji wa taulo za kike Juni 16,2025




Mwasilisha mada ya aina za ukataili wa Kituo cha Taarifa na maarifa Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Sophia George akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili na nne Katika Shule ya Sekondari Isoso kuhusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia kwenye maadhimisho wa siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na kituo hicho wakishirikaina na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Juni 16,2025





Mwakilishi wa Mkuu wa Shule ya Sekondari Isoso Kata ya Kishapu Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Madam.Jenipher Mushi akizungumza kwenye maadhimisho wa siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoratibiwa na kituo hicho wakishirikaina na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Juni 16,2025 yaliyofanyika katika shule hiyo kwa kutoa elimu na kugawa taulo za kike.




Social Plugin