Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWENGE WA UHURU KUZINDUA, KUWEKA MAWE YA MSINGI MIRADI 13 YA RUWASA YENYE THAMANI YA BILIONI 16.713

 

Na Hadija Bagasha- Tanga

JUMLA ya Miradi 13 katika Sekta ya Maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 16.713  inatarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Mkoani Tanga na itakayohudumia wananchi zaidi ya 85,017 hatua inayotajwa kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu ili kufuata huduma hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Juni 5 mwaka huu,  Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari Lugongo alisema kwamba miradi hiyo itanufaisha wananchi 85,017 ambao wanapata huduma ya maji safi na salama na kuondokana na adha ambazo walikuwa wanazipata awali.

Alisema kila Halmashauri itakuwa na mradi na miradi 6 ya uzinduzi,miradi 5 ya uwekeji mawe ya msingi katika miradi hiyo itakayozinduliwa itajumuisha vijiji 12 lakini kuwahudumia watu 28000 na karibia asilimia 1 ya wakazi wa mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba pia kuna miradi ya uzinduzi katika Jiji la Tanga kupitia Tanga Uwasa ambapo kutazinduliwa mita za malipo kabla na ni maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu ya viongozi wa chama na serikali ili kuhakikisha maji yanatumika kwenye viwango lakini yanatumika wananchi waweze kulipia kulingana na uwezo wao.

Aidha alisema kutakuwa na uzinduzi kwenye Jiji la Tanga ya Mita za malipo kabla 4,000 zitazinduliwa na mwenge pamoja  na kuwepo na miradi mengine ya uzinduzi kwenye wilaya za Handeni ,Lushoto ,Mkinga na mwengine utakuwa ni mradi wa uwekaji mawe ya msingi.

Alisema katika wilaya ya Pangani kwenye Jimbo la Waziri wa Maji kutakuwa na mradi wa uwekeji jiwe la msingi mradi wa maji Mkwaja ili uweze kukamilika kwa kipindi kifupi kijacho na katika miradi wanayoweka uzinduzi ni Kwedizinga wilaya ya Handeni Vijiji,Mgombezi Korogwe Mjini  na hapo wamejenga visima 900 vya Rais Samia Suluhu.

Aidha alisema kati ya visima hivyo ambavyo ni mradi maalumu wa kutatua changamoto ya maji kwenye maeneo yasiyokuwa na maji wilaya ya Korogwe watakuwa na mradi wa uzinduzi na wilaya ya Muheza watakuwa na mradi wa visima 900 watakwenda kuweka jiwe la msingi lakni watu wameshaanza kupata huduma ya maji ikiwemo wilaya ya Mkinga wanazindua mradi wa maji Gombero na wilaya ya Tanga ambazo  ni Mita za Luku za Maji na wilaya ya Lushoto ni mradi wa Funta –Wanga

Meneja huyo alisema pia kuna mirdi mitano ya uwekaji wa mawe ya msingi kwenye eneo la Kwamaligwa wilaya ya Kilindi ambao utahudumia vijiji saba na mradi wa Maji kwamahizi ambao utahudumia eneo la Handeni Mjini.

Alieleza pia Mwenge huo utatembelea mradi wa ukarabati miundombinu ya maji Lushoto Mjini ambao utaboresha huduma kwa wakazi zaidi 23,000 na uwekeji jiwe la msingi mradi wa maji Mkwaja na Visima 900 wa Rais kwa wilaya ya Muheza ambapo miradi hiyo yote inakwenda kuwahudumia wakazi wa Tanga asilimia 3 hivyo wanategemea miradi hiyo itakapokamilika itasaidia kuboresha asilimia 3.3 ya wakazi wa Tanga wakati ile asilimia 1 ya miradi itakayozindua nayo inakuwa imeshakamilika.

“Nimpongeze Rais Dkt Samia Suluhu kwa utekelezaji wa miradi hii pamoja na Mkuu wa Mkoa kwa kuendelea kutuongoza vema katika mkoa wetu pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa huu Rajab Abdurhaman"  alisema

Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuwasili Mkoani Tanga Juni 6 mwaka huu na kukimbizwa katika maeneo mbalimbali kwenye Mkoa huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com