Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MISA - TAN, EWURA WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI


MISA TAN kwa kushirikia na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendeshasSemina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu EWURA pamoja na majukumu yake.

Semina hiyo imefanyika leo Jumatatu Juni 16,2025 Jijini Dar es salaam na Nyirabu Musira kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA, ambapo amesisitiza umuhimu wa waandishi wa habari kuelewa kazi na majukumu ya EWURA ili waweze kuhabarisha jamii kwa usahihi na ufasaha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Edwin Soko ameishukuru EWURA kwa hiyo hiyo, akisema kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano baina ya mamlaka hiyo na vyombo vya habari nchini.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo ambao ni wanachama wa MISA-TAN kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Pwani, Dar es Salaam na Shinyanga, wameahidi kuzingatia yale wanayojifunza kupitia mawasilisho mbalimbali na kwenda kuyatekeleza kwa vitendo katika kazi zao za kila siku za uandishi wa habari.

Semina hiyo imelenga kuimarisha uelewa wa wanahabari juu ya mfumo wa udhibiti wa sekta ya nishati na maji nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com