Na Sofia Jumbe, Dodoma
Maiko Salali, amejiweka rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Jimbo la Mpwapwa katika uchaguzi ujao.
Salali alichukua fomu hiyo leo katika ofisi ya CCM Wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma, mbele ya viongozi wa chama, wanachama na wafuasi wake waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.
Maiko Salali anajiunga na orodha ya wanachama wa CCM wanaowania ridhaa ya kugombea ubunge kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, huku Jimbo la Mpwapwa likitarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mvuto wake wa kisiasa.
Social Plugin