Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA KUSIKILIZA KESI YA TUNDU LISSU 'Live' MOJA KWA MOJA MITANDAONI

Mahakama ya Tanzania imetangaza kuwa mashauri ya jinai namba 8606/2025 na 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu yatasikilizwa Jumatatu, 2 Juni 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Mashauri hayo yatarushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya Mahakama (www.judiciary.go.tz) ili kuruhusu wananchi kuyafuatilia bila kuhudhuria mahakamani.

Ukumbi wa Mahakama utachukua watu wachache tu, hivyo Wananchi wanahimizwa kufuatilia kesi kupitia mitandao kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya kuimarisha uwazi na matumizi ya TEHAMA.

Matangazo ya moja kwa moja yataanza kabla ya saa 2:30 asubuhi. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com