
Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Peter Mashenji akizungumza kwenye ziara ya Kamati ya siasa ya Wilaya kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kuona utekelezaji wa ilani ya Chama hicho.Picha na Sumai Salum
Na Sumai Salum-Kishapu
Kamati ya siasa ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo kwa lengo la kuona utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza katika ukaguzi wa miradi hiyo Kaimu mwenyekiti wa CCM Wilaya Mhe.Peter Francis Mashenji amesema miradi yote inaridhisha katika mwenendo wa utekelezaji wake na kuongeza kuwa uko wajibu wa kuongeza kasi ili ikamilike kwa haraka huku wakizingatia ubora wa ujenzi.
Miradi ya maji inayotekelezwa na RUWASA
1.mradi wa maji ya Ziwa Victoria Kijiji cha Mwabusiga Kata ya Kishapu unaotekelezwa na Mkandarasi MIWI Constraction Co.Ltd ulioanza Januari 2025 na unatatajiwa kukamlika Septemba 2025 wenye tuamani ya Tsh.Milion 281,658,305 kutoka mfuko wa maji wa taifa(NWF) utakao wanufaisha Wananchi wapatao 2,415.
2.Mradi wa maji ya Ziwa Victoria Kijiji cha Ipeja Kata ya Itilima Mkandarasi wa mradi huo ni Corsyne Consult Limited muda wa mradi ni miezi 6 na utekelezaji wake unatarajia kukamilika Juni 30,2025 mpaka sasa una 98%na wananchi wameanza kupata huduma ya maji safi kupitia mradi huo.Gharama za mradi ni Tsh. Milion 381,742,714.50 wanufaika wa mradi huo ni wananchi wa Kijiji wapatao 1,200.
3.Mradi wa Maji ya Bomba Masanga-Ndoleleji lenye urefu wa Km 33.3 unaotekelezwa na mkandarasi Mponela Construction and Company Limited muda wa utekelezaji mradi ni Mwaka mmoja na unatarajia kukamilika Octoba 30,2025 na sasa umefikia 75%.
Mradi unagharama ya Tsh.Bilioni 2,357,568,787 fedha kutoka serikali kuu kupitia Program ya Malipo kwa Matokea (PforR) wanufaika wa Mradi huo ni Wananchi wa Vijiji vya Ndoleleji,Masanga,Mwampalo na Ng'wang'halanga wapatao 12,768.
AFYA
1.Zahanati ya Wela ilipokea kiasi cha Tsh.Milioni 50,000,000 kutoka serikali kuu kw ajili ya ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vya Zahanati mwa mwaka 2024/2025
2.Ujenzi wa Wodi maalumu (VIP) Hospitali ya Dr.Jakaya Kikwete Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh. Milioni 200,000,000 kutoka serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa wodi hiyo ulioanza Disemba 1,2024 unatarajia kukamilika Juni 31,2025.
Mradi upo hatua za ukamilishaji(Kufunga milango,kufunga mfumo wa maji safi na maji taka pamoja na kupaka rangi mkono wa mwisho)
3.Ujenzi wa matundu 5 ya vyoo Zahanati ya Wela,Halmashauri ilipokea kiasi cha Tsh.milion 25,000,000 fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa matundu 5 ya vyoo,Placenta pit na kichomea taka.
Mradi ulianza Machi 10,2025 na unatarajia kukamilika Julai 10,2025 ambapo hadi sasa mradi uko kwenye hatua ya lipu kwa jengo na hatua za mwisho za utendaji shimo la choo.
Miradi inayotekelezwa na TARURA
1.ujenzi wa daraja barabara ya Igaga-Dugushilu(Tsh.Milioni 128,500,000) unatarajiwa kukamilika Julai 25,2025 Mkandalasi ni Gladiators Investment Limited
2.Dugushilu-Uchunga ujenzi wa barabara na makalavati wenye jumla ya Tsh.Milioni 154 unaotarajia kukamilika ifikapo Julai 25,2025 wenye Km 5.6.
3.Maganzo-Shinyanga Vijijini fedha kutoka Benki ya dunia kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Muhumbu katika Kijiji cha Ikonongo Mkandalasi akiwa ni Kihamba Constraction Company Limited.
ELIMU
Ujenzi wa Karakana Shule ya Msingi Kanawa mwaka wa fedha 2024/2025 shule ilipokea Tsh.Milioni 54,000,000 ambapo Milion 50 zitatumika kujenga karakana ya elimu ya watu wazima na milion 4 ujenzi wa matundu 2 vya choo.
Karakana hiyo imefadhiriwa na kujangwa na Taasisis ya elimu ya watu wazima chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Tekinolojia kwa ufadhiri wa watu wa Korea (KOICA) ikilenga kuwahudumia kuwapa Vijana wa Kiume na Kike wenye umri wa miaka 14-19 waliokatisha masomo yao katika mfumo rasmi wa elimu ya Msingi na Sekondari kwa sababu mbalimbali ikiwemo ugonjwa,utoro,umasikini,kufukuzwa na mimba.
Mashenji amesema malengo ya miradi hiyo ni kuwasogezea huduma wananchi ili waepukane na adha mbalimbali ikiwemo kupata maji safi,salama na yenye kuwatosheleza,kupunguza na kuondoa magonjwa yatokanayo na matumizi ya maji yasiyo safi na salama,kutembea umbali mrefu kutafuta maji,kupata huduma za afya kwa haraka na wepesi na Uraisi wa usafiri wa kwenda kupata huduma za kijamii na kusafirisha mazao kwa urahisi kwenda kwenye masoko na minada.
"Ni kweli tumepitia miradi yote nishauri tu kasi ya utekelezwaji wake uongezeka huku muda wa ukamilishaji miradi uzingatiwe ili wananchi wetu wapate huduma haraka iwezekanavyo hatutaki kusikia muda wa kukamilisha mradi umefika na haujakamilika mtakwamisha shughuli za maendeleo kwa wananchi wetu wa Kishapu" ameongeza Mashenji

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Peter Mashenji (Kushoto) na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi wakiwa kwenye ziara ya Kamati ya siasa ya Wilaya kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa lengo la kuona utekelezaji wa ilani ya Chama hicho

Jengo la Zahanati ya Wela Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga




Daraja la Muhumbu lililoko Kijiji cha Ikonongo Kata ya Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga litakalounganisha Kata hiyo na Shinyanga Vijijini linalojengwa kwa fedha kutoka Benki ya dunia


Wajumbe wa Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, wataalamu wa Halmashauri na wakuu wa taasisi na vitengo wakiendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo


Jengo la karakana iliyoko Shule ya msingi Kanawa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga

















Social Plugin