
Mfanyabiashara na mmiliki wa Kampuni ya Jambo Food Products iliyopo Ibadakuli mkoani Shinyanga Salum Khamis Salum "Jambo" amechukua fomu kuomba ridhaa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa jimbo la Meatu mkoani Simiyu.
Fomu hizo za ugombea zimetolewa na katibu wa chama hicho Naboth Manyonyi wilayani Meatu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi.
Salum Khamis amewahi kuhudumu katika nafasi za ubunge katika jimbo hilo katika vipindi tofauti tangu mwaka 2005 alipogombea rasmi ubunge wa jimbo hilo.
Salum Khamis ambaye ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amekuwa akishika nyadhifa mbalimbali za kiuongozi ndani ya chama chake tangu mwaka 2000 alipokuwa mwenyekiti wa umoja wa vijana mkoa na hadi sasa akiwa mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa pamoja na kuwa mjumbe wa kamati ya siasa ya mkoa.
Social Plugin