Na mwandishi wetu
Chama Cha Mapinduzi kimewaonya makatibu na watendaji wa chama hicho kutowatoza fedha za michango wanachama wanaochukua fomu za kuwania nafasi za ubunge na udiwani.
Onyo hilo limetolewa leo hii jijini Dodoma na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CPA Amos Makalla alipozungumza na waandishi wa habari.
Makalla ametoa onyo hilo, baada ya kupatikana taarifa kuwa kuna baadhi ya watendaji hao wamewatoza wanachama fedha zaidi ya kiwango kilichoweka cha ada ya fomu ambacho ni shilingi 500,000 kwa ubunge na 50,000 kwa udiwani.
Social Plugin