Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

🎶 NYASANI AACHIA WIMBO MPYA “SAWA” AKIWA NA MR. BLUE

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva kutoka mkoa wa Shinyanga, Nyasani, amedondosha rasmi ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la “SAWA” akiwa amemshirikisha mkali wa muda mrefu katika tasnia ya muziki Tanzania, Mr. Blue.

Wimbo huu mpya wa SAWA unakuja kama zawadi kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya, ukiwa umebeba ujumbe mzito wa maisha, mapenzi na matumaini, huku ukisindikizwa na melody tamu na beat za kisasa zilizotengenezwa kitaalam kwa ubora wa hali ya juu.

Mr. Blue, ambaye ni mmoja wa nguli waliotawala jukwaa la Bongo Fleva kwa zaidi ya miaka 15, ameongeza ladha ya kipekee katika wimbo huu. Ushirikiano wake na Nyasani umeibua hisia kali miongoni mwa mashabiki, na kuifanya kolabo hii kuwa kati ya zile zinazozungumzwa sana kwa sasa.

Kupitia “Sawa”, Nyasani anaonesha ubunifu na uwezo mkubwa wa kisanaa, huku akiendeleza harakati za kuitangaza Kanda ya Ziwa katika ramani ya muziki wa Tanzania.
🎥 TAZAMA VIDEO MPYA HAPA:

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com