Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Damas Ndumbaro akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Bombambili uliopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Utawala bora
Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Damas Ndumbaro akizungumza na wananchi katika ukumbi wa Bombambili uliopo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wakati wa Mafunzo ya Elimu ya Utawala bora
Wajumbe waliohudhuria kupata mafunzo ya Msaada wa Kisheria wa Mama Samia (Samia Legal Aid)
Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa Damas Ndumbaro, amekanusha vikali tuhuma za rushwa zinazodaiwa kutolewa kwa wananchi wakati wa mafunzo ya msaada wa kisheria yajulikanayo kama Samia Legal Aid.
Akizungumza leo tarehe 13 Mei 2025 wakati wa mafunzo hayo kwa viongozi wa chama, Waziri Ndumbaro amesema baadhi ya watu wamekuwa wakieneza taarifa potofu mitandaoni wakidai kuwa anahonga wananchi.
Mheshimiwa Ndumbaro ameeleza kuwa madai hayo hayana msingi wowote na yanatolewa na watu wenye nia ya kuchafua juhudi za serikali na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuelimisha jamii juu ya haki za kisheria.
“Kuna watu wanaishi humu humu mjini, hawataki mfaidike na mafunzo haya.
Wamediriki hata kuandika mitandaoni kuwa tunatoa rushwa.
Je, nani kati yenu amewahi kupewa rushwa?” amehoji mbele ya wanachama wa chama hicho.
Aidha, Waziri huyo amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa wakipotosha hata malipo ya nauli kwa washiriki wa mafunzo hayo kwa kuwaita rushwa.
Amefafanua kuwa malipo hayo ni kwa ajili ya kuwezesha ushiriki wa wananchi na siyo njia ya kununua uungwaji mkono kama inavyodaiwa na baadhi ya wakosoaji.
Amesisitiza kuwa kila anayepokea huduma hiyo anapaswa kuelewa kuwa ni haki yake kupata msaada wa kisheria.
Mheshimiwa Ndumbaro ametoa wito kwa wanachama na wananchi kwa ujumla kupuuza maneno ya watu wenye chuki na wivu wa maendeleo.
"Ukiona mtu ana kipato kizuri, cheo kizuri, lakini bado anakuharibia jina au kukuonea wivu — huyo ni mchawi,” ameongeza kwa msisitizo.
Amesema serikali itaendelea kutoa mafunzo na msaada wa kisheria kwa wananchi bila woga wala hofu ya maneno ya wapinga maendeleo.
Social Plugin