Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Wilaya ya Kahama Moses Job Kitula aliebeba shajala akiwakaribisha wananchi wote wa Manispaa ya Kahama na viunga vyake kushiriki katika mkutano mkubwa wa injili utakaoanza, tarehe 28 Mei 2025, na kudumu kwa siku tano.
NA NEEMA NKUMBI - KAHAMA
Mwenyekiti wa umoja wa Makanisa ya Kipentekoste (CPCT) Wilaya ya Kahama Moses Job Kitula amewakaribisha wananchi wote wa Manispaa ya Kahama na viunga vyake kushiriki katika mkutano mkubwa wa injili utakaoanza tarehe 28 Mei 2025, na kudumu kwa siku tano.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 27, 2025, Mwenyekiti huyo amesema maandalizi yote yamekamilika na tayari wageni waalikwa kwa ajili ya mkutano huo wamewasili.
Mkutano huo utaanza Mei 28 asubuhi kwa semina ya Neno la Mungu itakayofanyika kuanzia saa 1:00 asubuhi katika kanisa la Shalom Temple na baada ya semina hiyo, shughuli za mkutano wa injili zitaendelea katika Uwanja wa Magufuli uliopo eneo la Majengo, Manispaa ya Kahama.
“Nawakaribisha watu wa dini zote na rika zote kushiriki nasi katika mkutano huu wa kiroho, Tuanze na semina ya Neno la Mungu saa 1:00 asubuhi katika kanisa la Shalom Temple, kisha tuhamie katika viwanja vya Magufuli kuendelea na mkutano wa injili,” amesema Mwenyekiti huyo.
Mkutano huo unatarajiwa kuwaleta pamoja maelfu ya wakazi wa Kahama na wageni kutoka maeneo mbalimbali, kwa ajili ya kushiriki ibada, maombi, na mafundisho ya Neno la Mungu.
Social Plugin