Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili taarifa za kamati za kudumu kipindi cha robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025 April 30,2025 katika ukumbi wa mikutano alipokuwa akijibu hoja kuhusu mipango ya serikali kudhibiti ndege waharibifu wa mazao ya nafaka aina ya Kweleakwelea waliosababisha upotevu wa tani 150 za nafaka Wilayani humo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Willium Jijimya akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili hoja za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa za kamati za kudumu robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025
****
Na Sumai Salum-Kishapu
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson amewataka maafisa kilimo Wilayani humo kuwa karibu na wakulima ili wabaini kwa haraka changamoto wanazokutana nazo.
Johnson ameyasema hayo April 30,2025 Kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa kujadili taarifa za kamati za kudumu kipindi cha robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025.
"Nikiri wazi mbele ya baraza hili kuwa Wilaya yetu imekumbwa na ndege waharibifu aina ya Kweleakwela na kusababisha hasara kubwa ya uharibifu wa mazao ya nafaka kwa wananchi wetu hivyo mimi na wataalamu wangu tulishatoa taarifa kwenye mamlaka husika ya udhibiti mimea na viuatilifu Tphpa na wakalifanyia kazi" ,amesema Johnson
Mkurugenzi huyo amewataka maafisa kilimo ngazi zote kuhakikisha wanaendelea kuwa karibu na wakulima kwa kuwapa elimu bora ya ulimaji wa kisasa na kuzingatia kanununi zote za kilimo ili kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabiri kwa haraka ikiwemo wadudu na ndege waharibifu na serikali isaidie mapema kuondoa uharibifu utakaopelekea upungufu wa chakula.
"Na bado tunawasiliana na watalamu wa mamlaka husika ili kama bado kunamahali kweleakwelea wanasumbua waje wawashughulikie ili wakulima wapate faida kwenye kilimo walichowekeza" ameongeza Matinyi.
Kauli hiyo ya Mkurugenzi imefuatia baada ya muwasilishaji wa taarifa ya uchumi,ujenzi na mazingira Mhe.Fednand Mpogomi kuhoji kuhusu jitihada za serikali kuendelea kutokomeza ndege hao waharibifu.
Afisa kilimo Msimamizi wa zao la mpunga na pembejeo Wilaya ya Kishapu Steven Chande amesema ndege hao wamevamia na kuathiri maeneo ya tarafa zote Kishapu,Mondo na Negezi na kuathiri mazao ya nafaka ikiwemo mpunga, mtama na uwele hekali 400.
"Uharibifu huo umepelekea wakulima kupata upungufu wa mazao yaliyokuwa yakielekea kukomaa ambapo takribani tani 150 zilizotarajiwa kuvunwa zimepotea kwa wakulima wa mazao ya nafaka katika Wilaya yetu", amesema Chande
Jitihada za awali za kukabiliana na ndege hao waharibifu ni pamoja na Wakulima kuhamia kwenye mashamba yao na mamlaka ya udhibiti mimea na viuatilifu Tphpa Arusha wametoa ndege kwa ajili ya unyunyuziaji viuatilifu vya kudhibiti ndege waharibifu Kweleakwelea huku hadi sasa imeshafanya kazi katika tarafa zote tatu.
Mkulima wa mazao ya nafaka,alizeti na pamba Paschal Januari kutokea Kata ya Ndoleleji amesema Kweleakwelea wameathiri kwa kiwango kikubwa shamba lake la mpunga na wakulima wengine hivyo ameiomba serikali kuongeza jitihada za kuangamiza ndege hao kwa mara nyingine kwani wanapata hofu ya kukosa chakula kwa kiwango walichotaraji licha ya nguvu kazi kubwa waliyoiwekeza.
Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mhe.Richard Dominiko akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kwenye baraza la madiwani la Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mwakilishi wa taarifa ya kamati ya uchumi,ujenzi na mazingira Mhe.Fednand Mpogomi alieyeibua hoja ya uwepo wa ndege aina ya Kweleakwelea wanaoathiri mazao ya nafaka kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa kamati za kudumu.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe. Francis Manyanda akizungumza kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa za kamati za kudumu robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Shija Malisha Ntelezu akizungumza kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili taarifa mbalimbali za kamati ya kudumu katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo Aprili 30,2025
Mjumbe wa kamati ya fedha,utawala na mipango Mhe.Edward Manyama akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili taarifa za utekelezaji shughuli mbalimbali za maendeleo robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025 lililofanyika April 30,2025.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Mkoani Shinyanga Godwin Everygist akiwasilisha taarifa ya lishe ya Wilaya kwenye mkutano wa baraza la madiwani la kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ya Kata robo ya tatu mwaka wa fedha 2024/2025
Afisa kilimo msimamizi wa zao la mpunga na pembejeo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Steven Chande akizungumzia uharibifu uliosababishia wakulima hasara ya mazao ya nafaka kutokana na ndege aina ya Kweleakwelea kushambulia mazao yao.
Mkulima wa mazao ya nafaka,alizeti na pamba kutoka Kata ya Ndoleleji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Paschal Januari akizungumzia jinsi Kweleakwelea walivyohatarishi kwa mazao ya nafaka waliyotarajia kuwa msaada wa chakula na kiuchumi pia.
Social Plugin