TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE: 28 MEI 2025
WAANDISHI WA HABARI 8 WAIBUKA KIDEDEA TUZO ZA UMAHIRI KATIKA UANDISHI WA HABARI ZA TAKWIMU ZANZIBAR
· Redio jamii Pemba zaibuka kidedea kwa kuendeleza misingi ya usawa wa kijinsia, wakifuatiwa na gazeti la Zanzibar Leo
· Asya Hassan wa Zanzibar Leo aibuka mshindi wa Jumla
· Waandishi chipukizi nao wang’ara.
Jumla ya waandishi wa habari wanane (8) na vyombo vya habari vitatu (3) wameibuka kidedea katika tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari za Takwimu za wanawake na uongozi zilizoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali (OCGS) pamoja na Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA) na Jumuiya ya Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO).
Miongoni mwa vipengele vilivyoshindaniwa ni kipengele cha radio, kipengele cha magazeti, kipengele cha mitandao ya kijamii, kipengele cha waandishi wa habari vijana (YMF) na kipengele cha vyombo vya habari vyenye kuendeleza na kukuza usawa wa kijinsia.
Kati ya washindi hao wanane, watano miongoni mwao walitoka katika kipengele cha waandishi wa Habari vijana ambao walitambuliwa kwa kuzawadiwa vyeti pamoja na iPad kwa kila mmoja. Washindi hao ni:
- Salum Ameir Salum
- Zurima Ramadhan
- Nihifadhi Abdulla Issa
- Fatma Hamad Faki
- Maryam Nassor Suleiman
Vilevile, Asya Hassan Bakar kutoka gazeti la Zanzibar Leo aliibuka kuwa mshindi wa jumla na mshindi katika kipengele cha gazeti, alizawadiwa cheki ya shilingi Milioni moja na Laki tano, cheti pamoja na trofi, mwengine ni Huwaida Nassor Moh’d kutoka Assalam Fm Radio ambae amekua mshindi wa kwanza katika kipengele cha Redio nae alizawadiwa cheki ya Shilingi milioni moja, cheti pamoja na trofi na mshindi wa kwanza katika kipengele cha mitandao ya kijamii ni Salum Ameir Salum alipokea cheki ya Shilingi milioni moja, cheti pamoja na trofi
Kwa upande wa Vyombo vya Habari jumla ya vyombo vitatu vya habari vilitambuliwa kwa juhudi zao katika kuendeleza na kukuza usawa wa kijinsia kwenye kazi zao za kila siku, vyombo hivyo vilizawadiwa cheki ya Shilingi milioni mbili (2,000,000) kwa kila kimoja pamoja na vyeti vya shukran. Vyombo vya habari vilivyoibuka washindi ni:
- Redio Jamii Micheweni.
- Redio Jamii Mkoani.
- Shirika la Magazeti ya Serikali.
Waandaaji wa Tuzo hii wanatoa wito kwa waandishi wa habari wa na vyombo vya Habari kuendelea kuandika habari zinazohusu takwimu za wanawake na uongozi, kusimamia na kukuza usawa wa kijinsia, kuelezea mazuri yanayofanywa na wanawake na vikwazo mbalimbali vinavyowazuia wanawake wasifikie nafasi za uongozi.
Jumla ya kazi 235 kutoka vyombo vya habari vya aina zote vikiwemo magazeti, redio, televisheni pamoja mitandao ya kijamii, ziliwasilishwa kwa ajili ya kushindanishwa, ambapo jumla ya kazi 120 zilikabidhiwa kwa majaji kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi na hatimae kupatikana washindi hao.
Tuzo hizi ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Kuwawezesha Wanawake kushika nafasi za uongozi (SWIL), ambayo inatekelezwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar (TAMWA ZNZ), Jumuiya ya Wanawake wenye Ulemavu Zanzibar (JUWAUZA), Jumuiyay a Mazingira, Jinsia na Utetezi Pemba (PEGAO) na Jumuiyay a Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), kwa ushirikiano na Ubalozi wa Norway nchini Tanzania.
Imetolewa na:
TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
PRESS RELEASE
Date: 28th May 2025
8 JOURNALISTS EMERGE WINNERS IN THE DATA JOURNALISM AWARDS.
· Community radio in Pemba lead in promoting gender equality, followed by Zanzibar Leo newspaper
· Asya Hassan of Zanzibar Leo crowned overall winner
· Emerging young journalists also shine
A total of eight (8) journalists and three (3) media outlets have emerged winners in the Data Journalism Awards focusing on women and leadership. The awards were organized by the Tanzania Media Women’s Association – Zanzibar (TAMWA ZNZ) in collaboration with the Office of the Chief Government Statistician (OCGS), the Association of Women with Disabilities Zanzibar (JUWAUZA), the Zanzibar Female Lawyers Association (ZAFELA), and the Pemba Environment, Gender and Advocacy Organization (PEGAO).
Award categories included radio, newspaper, social media, young media fellows (YMF), and media institutions promoting gender equality.
Out of the eight winners, five were recognized under the young media fellows’ category and were awarded certificates and an iPad each. These winners are:
1. Salum Ameir Salum
2. Zurima Ramadhan
3. Nihifadhi Abdulla Issa
4. Fatma Hamad Faki
5. Maryam Nassor Suleiman
Asya Hassan Bakar from Zanzibar Leo Newspaper emerged as both the overall winner and the winner in the newspaper category. She received a cheque for TZS 1.5 million, a certificate, and a trophy.
Another winner, Huwaida Nassor Moh’d from Assalam FM Radio, won in the radio category and received a cheque of TZS 1 million, a certificate, and a trophy.
In the social media category, Salum Ameir Salum was awarded and received a cheque of TZS 1 million, a certificate, and a trophy.
Regarding media houses, three media houses were recognized for their continued efforts in promoting gender equality in their daily work. Each was awarded a cheque of TZS 2 million and a certificate of appreciation. The awarded media outlets are:
· Micheweni Community Radio
· Mkoani Community Radio
· Corporation of Government Newspapers
The organizers call upon journalists and media outlets to continue producing stories that focus on women and leadership statistics, promoting and upholding gender equality, highlighting the achievements of women, and uncovering barriers that hinder women from accessing leadership positions.
A total of 235 entries from various media including newspapers, radio, television, and social media were submitted for the competition. Of these, 120 entries were forwarded to the panel of judges for review, which resulted in the final selection of winners.
These awards are part of the implementation of the Strengthening Women in Leadership (SWIL) program, which is jointly implemented by TAMWA ZNZ, JUWAUZA, PEGAO, and ZAFELA, in collaboration with the Royal Norwegian Embassy in Tanzania.
Issued by:
TAMWA ZNZ, JUWAUZA, ZAFELA & PEGAO.
Social Plugin