Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROF. JANABI ACHAGULIWA KUWA MKURUGENZI WA WHO KANDA YA AFRIKA


Tanzania imeandika historia! Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, katika uchaguzi uliofanyika leo jijini Geneva, Uswisi.


Prof. Janabi anachukua kijiti kilichoachwa na Dkt. Faustine Ndugulile, Mtanzania mwenzake aliyefariki dunia mwezi Novemba 2024, na kuacha pengo kubwa katika uongozi wa afya barani Afrika.

Katika kinyang’anyiro hicho chenye ushindani mkali, Prof. Janabi aliwashinda wagombea kutoka mataifa mbalimbali akiwemo:
Prof. Moustafa Mijiyawa (Togo),
 Dkt. N’Da Konan Michel Yao (Ivory Coast),
Dkt. Boureima Hama Sambo (Niger), na
Mohamed Lamine Dramé (Guinea)

Kwa mujibu wa kanuni za WHO, Prof. Janabi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano, akiwa na uwezekano wa kuchaguliwa tena kwa muhula mmoja wa nyongeza.

Uchaguzi huu ni ushuhuda wa heshima ya kimataifa kwa mchango wa Tanzania katika sekta ya afya, na ni motisha kwa wataalamu wa ndani ya nchi kuwa ndoto zao zinaweza kufika mbali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com