Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CCM SHINYANGA YAPONGEZA MAENDELEO BUNAMBIYU, YAPANDA MITI KUADHIMISHA WIKI YA WAZAZI

Na Sumai Salum - Kishapu

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, ameongoza ziara ya kukagua miradi ya elimu katika Shule ya Sekondari Bunambiyu, wilayani Kishapu, na kupongeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya elimu.

Katika kipindi cha miaka mitano, shule hiyo imepokea zaidi ya Tsh milioni 166 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi, na matundu ya vyoo, ikionesha mafanikio makubwa ya uwekezaji wa serikali kwenye elimu.

Akiongozana na viongozi wa chama na Jumuiya ya Wazazi, Mhe. Mlolwa amepanda miti katika mazingira ya shule hiyo kama ishara ya utunzaji wa mazingira na kuadhimisha wiki ya wazazi mkoa wa Shinyanga.

Maadhimisho hayo yanaendelea kwa kutoa elimu juu ya malezi, maadili na afya ya familia.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akiwasili katika shule ya sekondari Bunambiyu akiwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Shinyanga John Siagi.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akipanda mti katika shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akipanda mti katika shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga John Siagi akipanda mti katika Shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wili ya wazazi Mkoa wa Shinyanga.
Picha na Mapuli Misalaba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com