Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDUMBARO: ALIYOYAFANYA RAIS SAMIA HAYAITAJI UVAE MIWANI YAPO WAZI


Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa

Na Lydia Lugakila

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dkt. Damas Ndumbaro amesema maendeleo aliyoyafanya Rais Samia karibu kila sehemu hapa Nchini yanaonekana wazi hivyo  hayahitaji mtu kutumia miwani ili ayaone.

Dkt.Ndumbaro amesema hayo wakati wa ufunguzi wa kampeini ya kisheria ya Mama Samia(MSLAC) iliyofanyika April 14  katika viwanja vya mashujaa maarufu  Mayunga vilivyopo Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Akiwahutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kuleta changamotoo zao zinazohitaji msaada wa kisheria Dkt. Ndumbaro amesema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna alivyoendelea kuwajali wanakagera na Watanzania kwa ujumla katika mambo mbali  mbali ya maendeleo aliyoyafanya ambayo hata hayahitaji mtu utumie miwani kuyaona.

Waziri Ndumbaro amesema kuwa Rais Samia amefanya mambo makubwa yanayoonekana wazi muhimu zaidi ikiwa ni katika sekta ya sheria na sekta ya haki ambapo ametenda mema sana.

"Kwa upande wa muindombinu tumeona majengo mbali mbali yanajengwa juzi tumezindua jengo kubwa la mahakama barani Afrika,na katika mikoa mbali mbali kuna majengo yanajengwa katika sekta hii" alisema Waziri Ndumbaro.

Amesema kuwa katika uteuzi wa waheshimiwa majaji hakuna Rais katika historia ya Nchi hii ameteua majaji wengi   kama Rais Samia na kuwa hali hiyo inasaidia Wananchi kupata haki kwa wakati na kupunguza mrudikano wa mashauri mahakamani na kupunguza pia mrundikano wa maabusu gerezani.

Amesema kuwa si hiyo tu bali Rais Samia ameunda time ya haki jinai yenye lengo la kuhakikisha kila Mwananchi au Mtanzania anapoingia katika mfumo wa haki jinai anaweza kushughulikiwa kwa usawa.

"Rais Samia ametekeleza ibara ya 13 kwa kuleta msaada wa kisheria ambao sasa mnaona umetua Kagera tumieni huduma hii ili iwatatulie changamoto zenu" alisema kiongozi huyo.

Ameongeza kuwa mnamo mwaka 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga sheria namba 1 ya mwaka 2017 sheria ya utoaji wa msaada wa kisheria na kuwa kufikia hatua hiyo Rais Samia amepata sifa ya kuwa kiongozi aliyeiheshimu katiba na sheria.

Ameongeza kuwa Serikali imeajiri maofisa madawati zaidi ya 400 Nchi nzima watakaoshughulikia malalamiko ya kisheria hivyo kampeini hiyo ninendelevu.

"Tutamlipa nini huyu Mama Samia tumuombee Sana apate  ushindi wa kishindo Oktoba 2025 na kama kuna mtu au watu wanataka kuweka mpira kwapani ruksa lakini mechi haihairishwi iko pale pale "alisema Waziri Ndumbaro.

Aidha ameongeza kuwa Serikali imeongeza  Taasisi za utoaji msaada wa kisheria 3,77 mpaka sasa kutoka 84 tangu Rais Samia anaingia madarakani.

Amewahimiza viongozi wa dini mkoani Kagera kutumia njia ya mbadala  ya utatuzi migogoro  badala ya kukimbilia vyombo vya sheria kila wakati huku akiwataka watendaji wa vijiji na wenyeviti kutatua migogoro na si kuzalisha migogoro ambapo pia
amezitaka familia kutafuta muafaka kwani familia nyingi ndizo chimbuko la migogoro mingi  ya ardhi na mirathi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma  Mwassa amesema kuwa Serikali Mkoani humo haitasita kumvua uenyekiti mamlaka wenyeviti wa vijiji na mitaa pamoja na kuwatengua watendaji wa mitaa na vijiji wanaosabanisha migogoro ya ardhi kutokana na kubaini kuwa viongozi hao ni chanzo cha kusababisha migogoro hiyo baada kuuza ardhi bila utaratibu maalum.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com