Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAWAPONGEZA WALIPAKODI BORA WA MKOA WA SHINYANGA NA MKOA WA KODI KAHAMA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Anamrigi Macha
Emmanuel Nnko mwakilishi wa Kamishina mkuu wa TRA Taifa ,ambaye ni Mkurugenzi wa TEHAMA ,TRA .
Na Patrick Mabula , Kahama

Serikali mkoa wa Shinyanga imewapongeza wafanyabiashara kwa kuwa na mwamko wa kulipa kodi hali inayofanya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuvuka malengo ya ukusanyaji wa kodi.

Pongezi hizo zimetolewa Februari 28,2025 na Mkuu wa mkoa wa Shinyanga , Anamrigi Macha katika sherehe ya utoaji wa wa Tuzo kwa walipa kodi bora wa mwaka 2023/2024 wa mkoa wa Shinyanga na mkoa wa kikodi wa Kahama iliyofanyika ukumbi wa Malex mjini Kahama.

Macha amesema amewapongeza kwa mwamko na uhiari wao wa kulipa kodi kwa hiari na kwa mujibu wa sheria kuunga mkono juhudi za serikali katika suala la ukusanyaji wa mapato unaofanywa na TRA.

“ Ndugu zangu wafanyabiashara na wajasiriamali wadogowadogo mnapaswa mtambue kuwa kulipa kodi ni wajibu wenu kwa maendeleo ya Taifa letu kwa hiyo wito wangu timizeni takwa hilo kwa mjibu wa sheria na niwapongeze sana kwa mwamko huo", amesema Macha.

Macha katika hotuba yake amewataka wafanyabiashara wanao kidhi vigezo kwenda TRA kuzisajili biashara zao kwenye matumizi yamashine za EFD, ambapo ametoa onyo kwa wasiotoa risti sahihi za mashine hizo wanapouza bidhaa zao.


Awali katika taarifa yake muwakilishi wa Kamishina mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Emmanuel Nnko ambaye ni mkurugenzi wa Tehama amesema wanatambua mchango mkubwa wa walipa kodi wa mkoa wa Shinyanga na mkoa wa kikodi Kahama ambao pekee inawafanya wafikie malengo kwenye kukusanya kodi.


Amesema TRA kama taasisi inapimwa kiutendaji ambapo kwa mwaka 2023/2024 mkoa wa Shinyanga na mkoa wa kikodi Kahama walivuka lengo kwa kukusanya shilingi 34,105,615,707.59 ikiwa sawa na asilimia 132.05% ya lengo la kukusanya sh.25,777,339,635.00 iliyokuwa imepangwa kwa mwaka huo husika.



“ Naomba kuhimiza katika masuala mtambuka, katika jitihada mbalimbali za TRA , bado kuna changamoto kwa wafanyabiashara ya kutotumia mashine za EFD na matumizi sahihi na kukwamisha misingi mikuu ya kulipa kodi sahihi za biashara zao na kuisaidia TRA ukadiliaji sahihi kwa wa kodi, amesema Nnko.



Nnko ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaotumia mashine za EFD kuwajibika kutoa risiti sahihi wanapouza na wateja wanaponunua bidhaa kudai risiti sahihi ya huduma aliyopewa mahali popote hapa nchini kila mmoja awajibike kwa hilo.

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa kodi , mwenyekiti wa TCCIA  wilaya yq Kahama, Charles Machali na Nashon Yohana , Naibu Katibu wa shirikisho la Wamachinga mkoa wa Shinyanga wameipongeza Serikali na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya kulipa kodi na kuomba elimu iendelee kutolewa kwao zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com