
Katibu wa UVCCM mkoa wa Pwani Ndg. Iddi Ntonga amefanya ziara yake ya kazi wilayani Bagamoyo ambapo ametembelea vikundi ambavyo vimenufaika na mkopo wa asilimia nne 4 ya vijana unaotolewa na halmashauri zote nchini.
Pia ametembelea vikundi vya waendesha pikipiki (boda boda) na kuwatia moyo katika kazi zao.
"Umoja na ushirikiano na kufata sheria zote za usalama barabarani ndio nguzo ya usalama wetu, nasi kama viongozi tunaotokana na vijana tutajitoa kuwalinda na kuwatetea" ,amesema Ndg. Ntonga.
Aidha ametembelea shule ya sekondari Rupungwi iliyopo kata ya Mandera jimbo la Chalinze na kupata wasaa wa kuzungumza na wanafunzi kwa kuwasihi wasome kwa bidii na kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kuepuka wimbi la mmomonyoko wa maadili.
Social Plugin