Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TPA TANGA YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE NA WATOTO WA KITUO CHA GOODWILL


Na Hamida Kamchalla, TANGA.

KUELEKEA kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Dunia, wanawake wa Mamlaka ya Bandari ya Tanga, wameshiriki katika Iftari na watoto wa Kituo cha kulea watoto cha Goodwill kilichopo jijini Tanga.

Tukio hilo limefanyika jana katika viwanja vya Habours Club jijini humo likienda sambamba na kugawa msaada kwa watoto hao, ambapo walipatiwa vyakula vikiwemo Michele, maharagwe, mafuta, magodoro 20, mafuta ya kula pamoja na pesa taslimu sh lakini tano.

Wakati wa makabidhiano ya msaada huo, Ofisa Rasilimali na Utawala Bandari ya Tanga Sharifa Nuhu amesema wamekuwa wakifanya matendo ya huruma ya kibinadamu, na kwa mwaka huu kuelekea siku ya wanawake Duniani wameamua kutoa msaada na kuftari pamoja na watoto hao.

"Tulikwenda kituoni kwao kuwataka watuandikie orodha ya mahitaji yao, wakatupa na sambamba na msaada wa vyakula na magodoro pia tumemlipia mwanafunzi mmoja ambaye alikuwa na changamoto ya ada shuleni,

"Walitupa utaratibu wa kulipia shuleni na tukaingiza kwenye akaunti shule kiasi cha sh. Milioni 1.145, pesa taslimu sh lakini tano kwa ajili ya wanafunzi wengine kwa mahitaji ya nauli kwenda na kurudi shuleni", amesema.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwill Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi amesema ametoa shukrani zake na kuwaasa wakina mama wengine wenye uwezo wa kutoa japo kidogo katika sehemu yao kwani msaada kwa watoto wa sehemu za malezi nao uhitaji kama wengine.

Amesema wakina mama ndio walezi wa watoto hao, hivyo endapo watatoa kidogo walichonacho hata Mungu anawaongeza ijapo hawataweza kujua ni kwanini hawapungukiwi na kwamba kutilia shaka kwa kujitolea kwao ni mawazo ya Shetani.

"Sehemu za makao sio salama sana kwa watoto, kuwasaidia watoto waliokata tamaa ya maisha, wanaishi mazingira magumu haupotezi bali unajiwekea kwa Mungu, anayesema kusaidia watoto hawa hakuna maana, huo ni mpango wa Shetani", amesema.

Imekuwa ni kawaida kwa wakina mama wa Bandari ya Tanga kujitolea misaada kwenye vituo mbalimbali vya kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu,

Lakini kipindi hiki msaada huo wameutoa wakati muafaka wa kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani ikiambatana na maadhimisho ya wanawake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com