Na Barnabas kisengi Gairo.
Taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa wilayani gairo Mkoani Morogoro imetoa mafunzo kwa viongozi wa Dini Juu ya kuzuiya na kupambana na rushwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi Mkuu hapa nchini.
Akifungua mafunzo hayo February 25. 2025 Mkuu wa Takukuru wilaya ya Gairo Bi Julieth Mtuy amesema lengo la mafunzo hayo ni kujengeana uwezo wa pamoja kati ya viongozi wa Dini na taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa Takukuru ili kuweza kukabiliana na vitendo vya rushwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
"Tumeona TUANZE na kundi hili la Viongozi wa Dini kwakuwa wana nafasi kubwa ya kusikilizwa na waumini wao katika makanisa na misikitini Juu ya kupiga vita rushwa"amesema Bi Mtuy
Aidha Mkuu huyo wa Takukuru wilaya ya Gairo amesema kuwa elimu hiyo walio pata viongozi wa Dini itawafikia waumini kwa wakati kwakuwa viongozi na wanasiasa kila moja huwa anaamini Dini yake hivyo wameanza na Viongozi hao wa Dini katika wilaya yote ya Gairo kwa kuwapatia mafunzo hayo
Bi Julieth Mtuy amewataka Viongozi hao wa Dini kuwa nguzo Muhimu ya kupiga vita rushwa katika maeneo mbalimbali ili kuifanya tanzania kuwa Nchi ya amani na wananchi kuendelea kuipenda Nchi yao.
Kwa upande wake Afisa wa Takukuru wilaya ya Gairo Mohamed kimolo ameelazea juu mada ya nafasi ya viongozi wa Dini katika kuzuiya na kupambana rushwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa nafasi ya RAIS, wabunge na madiwani.
"Tunajua hivi karibuni nchi yetu itakuwa na uchaguzi Mkuu hivyo viongozi wa Dini mnapaswa sana kukemea vitendo vya rushwa katika maeneo yenu hivyo tukishirikiana kwa pamoja hakika tunafanikiwa kutokomeza rushwa"amesisitiza kimolo
Elimu ya mafunzo ya kuzuiya na kupambana na rushwa wilayani gairo Mkoani Morogoro yamelenga kufikia makundi mbalimbali katika kuelekea kipindi hichi cha Uchaguzi Mkuu hapa nchini.
Social Plugin