Na Barnabas kisengi Gairo
Elimu ya kuzuiya na kupambana na rushwa wilayani gairo Mkoani Morogoro inatarajiwa kuwafikia wananchi wote wa kata 18 zilizopo wilayani gairo Mkoani Morogoro kabla ya kwenda kwenye zoezi la kampeni za vyama vya Siasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka huu
Kauli hiyo imetole leo February 26,2025 na Mkuu wa taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa (Takukuru) wilaya ya Gairo Bi Julieth Mtuy wakati akizungumza na kituo hichi kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao wa nafasi ya RAIS wabunge na madiwani hapa nchini.
Bi Julieth Mtuy amesema wao kama ofisi ya Takukuru wilaya wameshajipanga kutoa Elimu ya kuzuiya na kupambana na rushwa wilayani gairo wakati wa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao.
"Sisi kama taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa tumekusudia kufikisha Elimu kwa wananchi wote wa wilaya ya Gairo kwa kutumia kliniki tembezi kwa kila kata lengo kubwa ni kuwaelimisha wananchi jinsi ya kuzuiya na kupambana na rushwa katika kipindi chote cha kampeni za vyama vya Siasa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao hapa nchini kwakuwa tukiwafikia huko walipo kwenye kata zao na vijiji na vitongoji vyao ili waepukane na dhana ya kupata kiongozi bora hadi wapewe rushwa hili jambo halikubaliki kabisa"amesisiza Bi Julieth Mtuy
Aidha Mkuu huyo wa Takukuru wilaya ya Gairo amesema kuelekea kampeni za vyama vya Siasa huwa kunajitokeza watu wachache wasio waadilifu na wazalendo wa Nchi wanakuwa wakitafuta vyeo kwa kutoa rushwa jambo ambalo ni kinyume cha sheria na katiba ya nchi yetu.
"Ukifika muda wa kampeni za vyama vya Siasa utaona baadhi ya watu wanaowania nafasi mbalimbali wanazitafuta nafasi hizo kwa kushawishi wananchi wawachague kwa sababu wanatoa rushwa Sasa kwa hapa Gairo wajipange kwakuwa tutawanasa tu sisi kama taasisi ya kuzuiya na kupambana na rushwa Takukuru kwa kushirikiana na vyombo vingine tumejipanga kuhakikisha swala la rushwa hatulipi nafasi hapa wilayani gairo hata kidogo"amesisiza Bi Julieth Mtuy
Mkuu huyo wa Takukuru wilayani ya Gairo amesema ndio maana sasa tunatarajia kuanzia kliniki tembezi ambayo itatembea kata zote 18 kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi Juu ya viashiria vya rushwa vikoje ili kuwajengea uwezo wananchi na viongozi kwenye kata zote ili kila moja apate uelewa na kuona rushwa ni adui mkubwa lazima tupige vita swala hilo.
"Hii kliniki tembezi naimani itatuletea mafanikio makubwa kabla ya kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu nasi kama taasisi tumejipanga vizuri kuhakikisha Elimu hii ya kuzuiya na kupambana na rushwa inafika kila kona na makundi mbalimbali wilayani hapa na tumeshaanza na kundi la Viongozi wa Dini na tutaendelea na makundi mbalimbali wilayani hapa yakiwemo wanasiasa,walemavu,wanawake, Mama lishe na Baba lishe,vijana na watu wenye ulemavu lengo ni kila moja ajue umuhimu wa kupinga rushwa katika maeneo yake"
Bi Julieth Mtuy amesema swala la rushwa ni swala mtambuka hivyo wao kama Takukuru watahakikisha macho na masikio wameyatega vizuri ili kuhakikisha wanawabaini wote watakao husika kutoa na kupakea rushwa kwani wote ni wakosaji.
Social Plugin