
🟢KIONGOZI NI MPATANISHI, MFARIJI NA KIONGOZI, HAKIKISHA WATU WANASHIBA KWANZA KABLA YA KUSHIBA WEWE
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Ndele Mwaselela Ametembelea Mkoa wa Songwe Kwa Siku Mbili Yaani Tarehe 23 Hadi 24/02/2025, Katika Wilaya ya Songwe na Momba (Tunduma) Kukutana na Makada na Viongozi wa CCM.
MNEC Mwaselela, Ameipongeza Serikali Inayoundwa na Chama Cha Mapinduzi, Ambayo Inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Kwa Miradi Mikubwa Inayotekelezwa Mkoani Humo.
MNEC Mwaselela, Amesema Tumejionea Fedha Nyingi Zikiletwa Mkoani Kwetu Songwe na Hivi Karibuni Zimeletwa Zaidi ya Bilioni 700 Ambazo Zitaenda kutekeleza Miradi Mbalimbali Katika Halmashauri Zetu, Kwaajili ya Kuleta na Kutengeza Mazingira Rafiki na Wezeshi Ili kuinua Uchumi wa Taifa na Wanasongwe Wote Kwa Ujumla Wetu, Hivyo Tunayo Kila Sababu ya Kumlipa Deni Hili na Kumuunga Mkono Kwa Kumpa Kura za Kishindo Hapo Mda Utakapofika.
Mwisho MNEC Mwaselela, Amesisitiza Kuwa Uongozi ni Utumishi Hivyo Lazima Kila Mtu Awe na Sifa ya Kuwa Mpatanishi, Mfriji na Kiongozi Anakuwa wa Mwisho Kushiba baada ya Watu Unaowaongoza Kwanza, na "kuepuka lugha ya vitisho wakati wote na Fitina. Kwakuwa Sifa Hizi zote Tayari Zimekwishaoneshwa na Mwenyekiti Wetu Wa CCM Taifa.
Aidha MNEC Mwaselela, Ameendelea Kusisitiza Kwa Kutolea Mfano Kwa Kunukuu Kutoka Kitabu Cha Mwalimu Nyerere Kiitwacho TUJISAHIHISHE Katika Ukurasa wake wa Pili Usemao "Kanuni Moja ya TANU inasema Nitasema Kweli daima. Fitina Kwangu ni Mwiko . Lakini Bado Tunao Wanachama Ambao ni Wafitini Wakubwa Bila Kijitambua. Ni Wa aina Mbalimbali. Wengine Humwona Mwanzao Anafanya Kosa. Badala ya Kumwambiya pale Pale Kijamaa Kwamba Utendalo ni Kosa, Watanyamaza Kimya. Lakini hawanyamazi Kabisa! Wataenda Kumteta Katika Vikundi vya Siri Siri. Matendo haya Si yakumsaidia Mwenzao ni ya Kumdhurumu. Hii ni Aina Moja ya Fitina na Wengine Hugawa Watu Katika Mafungu."
Lakini Pia Amezidi Kuwaasa Makada hao Kuzidi Kusoma Katiba ya CCM Ili Kuyatambua Malengo ya TANU na ASP Mpaka Kuungana Kwake na Kuwa na Lengo la Kuunda Chama Ambacho Kishike Barabara Hatamu za Uongozi wa Shughuli Zote za Umma Kwa Maslahi ya Wafanyakazi na Wakulima wa Taifa Letu na Chama Hiki Kitakachoundwa Kinatakiwa Kiwe Kiungo Cha Wanamapinduzi wa Tanzania na Wanamapinduzi Wenzetu Lolote Waliko.
MNEC Ameyasema hayo Alipokuwa Katika Wilaya ya Songwe na Momba (Tunduma) Katika Shughuli za Ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi Alipokutana na Viongozi na Makada wa CCM Mkoani Songwe.
#2025 ni Dkt.Samia na Dkt.Nchimbi
#Chama Imara, Serikali Imara
#Tunazima Zote, Tunawasha Kijani
Social Plugin