Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KAMPENI YA MAMA SAMIA YA MSAADA WA KISHERIA KUENDELEA KATIKA MIKOA MITANO

Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Damas Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini akizungumza leo na Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma.

Waziri wa Sheria na Katiba Dkt. Damas Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini akizungumza leo na Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma.


Na Regina Ndumbaro - Malunde 1 blog Ruvuma. 

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametangaza kuendelea kwa kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign (MSLAC), katika Mikoa Mitano. 

Ndumbaro amesema hayo leo Februari 15, 2025, Mkoani Ruvuma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema kuwa kampeni hii ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kutoa msaada wa kisheria, elimu ya msingi ya kisheria, na kusaidia utatuzi wa migogoro ya wananchi katika ngazi mbalimbali za jamii. 

“Hadi sasa, kampeni hii imetekelezwa katika mikoa 17 na itaendelea katika Mikoa mingine mitano katika awamu hii ambapo Uzinduzi wake unatarajiwa kuanza Februari 18, 2025 kwa  Mkoa wa Mwanza”, amesema Ndumbaro 

Aidha tarehe 19 Februari 2025, mkoa wa Lindi utafanya uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa atakuwa mgeni rasmi wa Uzinduzi huo

Ameongeza kuwa Februari 24, 2025, Mikoa mitatu ya Mbeya, Rukwa na Pwani itazindua rasmi kampeni ya Mama Samia Legal Aid.

Kwa mujibu wa Ndumbaro amesema ifikapo Machi 2025, kampeni hii itakuwa imekamilika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar, lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya msaada wa kisheria bila ubaguzi wowote. 

Kampeni ya Mama Samia Legal Aid inalenga kujenga jamii yenye maridhiano, ustahimilivu, mageuzi chanya, na taifa lenye amani.

 Pia, inatoa mafunzo ya utawala bora na sheria kwa ajili ya kujenga msingi thabiti wa utawala wa sheria nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com