Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JUMBE : TUNA KILA SABABU YA KUTAMBA NA RAIS SAMIA

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Mhandisi James Jumbe, amesema wananchi wa Shinyanga Mjini wana kila sababu ya kutamba na Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na mafanikio makubwa ya maendeleo yanayoendelea katika maeneo mbalimbali, hasa katika ujenzi wa miundombinu.

Akizungumza wakati wa ziara ya wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga Mjini, Jumbe alisisitiza kwamba miradi ya madaraja inayotekelezwa katika kata za Chibe na Ibinzamata ni ishara ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Alieleza kuwa Rais Samia ameonyesha kwa vitendo ufanisi mkubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara, jambo linalochochea maendeleo ya uchumi na kuboresha usalama na huduma kwa wananchi.

“Daraja la Chibe ni kubwa na zuri. Haya ni mambo mazuri yanayofanywa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan. Mama Samia ametekeleza Ilani ya CCM kwa zaidi ya asilimia 100. Ameonesha maendeleo ya kiuchumi kwa vitendo nasi hatuna zawadi ya kumpa zaidi ya kumpatia kura za kutosha kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2025 kwa sababu tayari Chama kimempitisha kuwa mgombea Urais kupitia CCM pamoja na mgombea mwenza Dkt. Emmanuel Nchimbi ili waweze kutuletea maendeleo zaidi,” amesema Jumbe.

 Mhandisi James Jumbe 

Jumbe amesisitiza kuwa ujenzi wa madaraja ya Chibe – Old Shinyanga na Ibinzamata Makaburini ni hatua muhimu katika kuboresha miundombinu ya barabara na usafiri katika wilaya ya Shinyanga. 

“Daraja hili limerahisisha mawasiliano kati ya kata ya Chibe na Old Shinyanga, kwa sababu hapa palikuwa hapapitiki wakati wa masika kutokana na kuwepo kwa mto mkubwa. Usalama sasa upo na mapato ya Halmashauri yameongezeka kutokana na kwamba sasa wafanyabiashara wengi wanaokwenda katika Mnada wa Old Shinyanga na Tinde wanapita katika daraja hilo,” ameeleza Diwani wa kata ya Chibe, Mhe. John Kisandu, ambaye alikuwepo kwenye ziara hiyo.

Kwa upande mwingine, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko, amesema kuwa ujenzi wa madaraja hayo ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kwamba miradi hiyo ni kielelezo cha namna fedha zinazotolewa na Rais Samia zinavyosaidia kuboresha miundombinu.

“Tumeliona daraja linalounganisha Chibe na Old Shinyanga, ni zuri, limejengwa na mhandisi mahiri, linaunganisha kata ya Chibe na Old Shinyanga na maeneo mengine kama Mwawaza hadi. Daraja hili ni zuri na tunaenda kuifanyia kazi ombi la diwani kuwekewa taa kwenye daraja hili ili kuimarisha usalama kwa wanaopita nyakati za usiku,” amesema Mrindoko.

“Tumejionea pia ujenzi unaoendelea wa daraja la Ibinzamata Makaburini. Daraja hili linajengwa vizuri. Tunawapongeza viongozi wote mliofanikisha kujengwa kwa daraja hili ili kurahisisha usafiri, lakini pindi tatizo la msiba linapotokea, wananchi waweze kupita kwa urahisi kwenda kuwahifadhi ndugu zetu waliotangulia mbele za haki. Ujenzi unaendelea vizuri na lipo katika hatua za ukamilishaji,” amesema Mrindoko.

Mrindoko ameipongeza Serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ya barabara, elimu, maji, afya n.k.

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakitembelea Daraja la Chibe - Old Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiwa katika daraja la Ibinzamata Makaburini

Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji  Jumuiya ya wazazi CCM wilaya Shinyanga Mjini wakiondoka katika daraja la Ibinzamata Makaburini
Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
Ujenzi wa daraja la Ibinzamata Makaburini ukiendelea
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na Viongozi wa CCM Kata ya Chibe

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com