RC RUVUMA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MIILI YA WALIMU WALIOFARIKI KWENYE AJALI
Friday, January 03, 2025
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas Ahmed
Na Regina Ndumbaro Ruvuma
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, ameongoza mamia ya waombolezaji katika Wilaya za Mbinga na Nyasa kwa ajili ya kuaga mabaki ya miili ya marehemu sita (6) waliokufa katika ajali ya gari iliyotokea Desemba 28, 2024. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya walimu wanne (4) pamoja na raia mmoja na dereva.
Katika hotuba yake, Kanali Ahmed alisema tukio hilo limemsikitisha sana, kwani limepoteza nguvu kazi ya taifa, wakiwemo walimu muhimu katika jamii. Alitoa wito kwa vyombo vya usalama barabarani kuongeza juhudi za ukaguzi wa vyombo vya moto na kutoa elimu ya mara kwa mara ili kuepuka ajali kama hizo.
Viongozi wa chama na serikali walihudhuria kwenye tukio la kuaga miili hiyo na walitoa salamu za pole kwa familia za marehemu.
Marehemu waliotambulika katika ajali hiyo ni: Vicent Alel Milinga (Dereva),Damas Damasi Nambombe (Mwalimu),Judith Joseph Nyoni (Mwalimu),John Silvester Mtuhi (Mwalimu) ,Dominic Abeat Ndau (Mwalimu) naBoniface Bosco Mapunda (Raia)
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin