TACOGA KUSHIRIKISHA TAASISI ZA ELIMU ZA CHINI MPANGO WA KUJENGA KIZAZI CHENYE MAADILI

Na Hadija Bagasha Tanga,

CHAMA cha Ushauri wa Wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati Tanzania (TACOGA 1984) kinafikiria kushirikisha taasisi za elimu za chini kwenye mpango wa kujenga kizazi chenye maadili kuanzia elimu ya awali msingi hadi vyuo vikuu, hatua hiyo inayokuja mara  baada ya kubainika maadili kwa jamii yameporomoka.

Hayo yameelezwa na  Mwakilishi wa katibu Mkuu Wizara ya elimu Akwila Sawaya ambaye ni Mdhibiti Mkuu Ubora wa shule kanda ya Kaskazini  Mashariki kwenye Mkutano wa Chama cha Ushauri wa Wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati unaofanyika katika jiji la Tanga ikiwa na dhamira  ya kujadili masuala mbalimbali ikiwemo masula ya jinsia na elinmu jumuishi kwa wanafunzi.

Amesema kwamba vyuo vikuu vinaweza kushiriki kujenga kizazi chenye maadili kinachoweza kuwa msaada kwa Taifa lakini pia wanaamini watafanya kazi kubwa ya kurejesha vijana wao kwenye tamaduni zinazokubalika na hatimaye kupata viongozi na wataalamu wazuri wenye maadili na wanaofata tamaduni za Tanzania.

“Chama kina malengo na lengo kubwa ndio hilo kama kuhakikisha kwamba elimu jumuishi inakuwepo lakini pia suala la maadili na tamaduni zetu zinazingatiwa kwa vijana wetu hivyo kinachotakiwa kufanya ni kushirikisha na shule nyingine taasisi za elimu za chini kwasababu kuna vyuo vya kati na vyuo vikuu lakini pia bado tunahitaji elimu wanayotoa ifike kwa vijana na watoto kuanzia shule za awali, msingi na sekondari,”alisema

“Changamoto kubwa ambayo imeonekena ni gharama za uendeshaji ni kubwa hivyo tutashirikisha wizara yetu kwa umuhimu wa jambo hili katika elimu kwakuwa hakuna elimu bila maadili huwezi ukasema unamtengeneza mwanafunzi kiakili lakini kimaadili akawa hayaendi sawa na utamaduni wa kitanzania,”alisisitiza

Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,Prof. Mohamed Makame Haji, ambaye pia ni mjumbe wa bodi ya wadhamini wa chama hicho amesema mkutano huo unaangalia kwa namna gani chama hicho kinaweza kuwa sehemu kuu ya  kutatengeneza wanafunzi na kuwa raia wema wanapohitimu mafunzo yao.

“Chama hiki kina mchango mkubwa sana katika kuwatengeneza wanafunzi ili kuwa wanafunzi bora ili wawapo katika vyuo na taasisi nyingine za elimu lakini pia kuwa raia wema wanapohitimu mafunzo yao na kutengeneza jamii ambayo ina uelewa na inayokwenda na maadili na kuwa na viongozi ambao watakuwa wasimamizi wazuri na wenye kujielewa,”alisema Prof.Makame.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha  cha Dodoma(UDOM),Prof.Lughano Kusiluka ,anasema jamii inatakiwa kusadia kujenga kizazi chenye maadili baaada ya dalili zilizopo kuonesha maadli yameporomoka kwa kiwango kikubwa.

Mkutano huo wa siku tatu,wa mafunzo maalumu  kuhusu elimu jumuishi  na mkutano mkuu wa  wa washauri  na wanasihi  wa wanafunzi  katika vyuo vya elimu ya juu  na kati TACOGA 1984 ,mumeshirikisha wajumbe zaidi na 108.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post