KILELE CHA WIKI YA VIZIWI DUNIANI KITAIFA YAFANYIKA SHINYANGA, VIZIWI WAOMBA WAKALIMANI LUGHA YA ALAMA

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Chama cha Watu Wenye ulemavu wa Kusikia Tanzania (CHAVITA) kimeadhimisha kilele cha wiki ya viziwi duniani ambapo kitaifa maadhimisho yamefanyika katika mikoa wa Shinyanga iliyobeba kauli mbiu isemayo 'Ungana kutetea Lugha ya alama'.

Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania na mjumbe wa Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA Mkoa wa Dar es salaam Bi. Tungi Mwanjara kwa niaba ya viziwi ameiomba serikali kuajiri wakalimani kwenye taasisi za umma na vyombo vya habari ili kusaidia watu wasiosikia kupata taarifa kamili na muhimu zinazoendelea nchini na dunia nzima.

Amesema hayo Leo tarehe Septemba 28, 2024 wakati akisoma risala kwenye maadhimisho ya wiki ya viziwi duniani iliyofanyika kitaifa katika uwanja wa Sabasaba manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.


"Tunaiomba serikali kuajiri wakalimani katika vyombo vya habari , hatupati habari kikamilifu vile inavyotakiwa kuna vyombo vya habari vingi hapa nchini havina wakalimani wa lugha ya alama hali inayofanya sisi tu viziwi kushindwa kapata taarifa kama ilivyo kwa watu wengine, kuna wakalimani ambao ni makanjanja hawajui lugha hii ya alama hao ndio wamekuwa wakitumiwa", 

"Hali hii ni kama kuwakandamiza viziwi kupata haki ya kujua kinachoendelea nchini na duniani, kushindwa kutoa nafasi za ajira kwa viziwi, sisi pia tunalipa kodi, kwenye kodi hizo waongezwe wakalimani," amesema Mwanjara.

"Changamoto wanayokumbana nayo viziwi ni kutokuwa na mawasiliano mazuri na watu ambao sio viziwi hasa kwenye sekta mbalimbali kama hospitalini, ofisi za serikali na binafsi kwa sababu hakuna wakalimani wa lugha za alama hivyo kusababisha viziwi kushindwa kupata huduma " amesema. 

Katika hotuba ya mgeni rasmi iliyotolewa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mhe. Patrobas Katambi kwa niaba ya Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa vyombo vya habari ni lazima viwe na wakalimani wa lugha ya alama ili kuwawezesha watu wasioweza kusikia kupata haki yao stahiki ya kuhabarishwa kama ilivyo kwa watu wengine huku akieleza hatua mbalimbali zilizofikiwa na serikali katika katika kuwatambua watumiaji wa lugha ya alama hapa nchini,

"Suala la kuajiri wakalimani sasa ni agizo la serikali na ni lazima vyombo vyote viajiri wakalimani kwa ajili ya kutoa taarifa sahihi kupitia lugha ya alama ambayo hii itawezesha wenzetu hawa kupata haki yao ya kimsingi ya kupata taarifa" ,amesema Katambi.

"Serikali imeenda mbali zaidi sio kwa lugha ya alama tu pia na lugha mguso kwa wenzetu wasioona, lugha hiyo imetafitiwa muongo wa elimu na pia serikali imetenga fungu kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa ngozi,ambapo kiasi cha shilingi milioni 104 kimetengwa kwa ajili ya mafuta ya watu wenye ualbino ili kupata mafuta hapa nchini na sio kuagiza mafuta kutoka nje",amesema Katambi.

Naibu waziri wa ofisi ya waziri mkuu kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Shinyanga mjini Mhe. Patrobas  Katambi kwa niaba ya Waziri wa kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu Tanzania na mjumbe wa Chama cha Viziwi Tanzania CHAVITA Mkoa wa Dar es salaam Bi. Tungi Mwanjara akisoma risala wakati wa maadhimisho hayo.














Picha ya maandamano ya wiki ya viziwi duniani.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post