AFISA ELIMU CHALINZE AHIMIZA CHAKULA KWA WANAFUNZI SHULENI

Mwalimu mkuu wa shule ya St. Alphonsa, Mtawa-Robson Mathew
Wahitimu wa elimu ya msingi mwaka 2024, shule ya msingi St. Alphonsa, Chalinze, Pwani
Mwenyekiti wa bodi ya shule, Bw. John Noah Kirumbi
AFISA elimu ya awali na msingi, halmashauri ya Chalinze, Bi. Miriam Kihiyo


NA. ELISANTE KINDULU,CHALINZE

AFISA Elimu ya awali na msingi wa halmashauri ya Chalinze Bi. Miriam Kihiyo ameitaka shule binafsi ya msingi ya St. Alphonsa kuangalia namna ya kuwapatia wanafunzi chakula cha mchana.

Bi. Miriam Kihiyo aliyasema hayo aliopokuwa akihutubia katika mahafali ya wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka 2024 katika shule hiyo jumamosi ya wiki hii.


Afisa elimu huyo amesema, utaratibu wa kuwapatia chakula wanafunzi ni mwongozo alioutoa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa shule kufanya utaratibu wa kuwapatia wanafunzi chakula nchini.


"Kaeni na bodi yenu ya shule muwaite wazazi ili waweze kuchangia chakula kwaajili ya watoto wao shuleni",alisema Bi. Kihiyo.


Bi. Kihiyo amewataka wazazi kutowaruhusu watahiniwa wa darasa la saba kupoteza muda kwenye luninga kuangalia tamthilia na kucheza gemu kwenye simu na badala yake watumie muda mwingi kujiandaa kwaajili ya mtihani wa Taifa.


Aidha afisa elimu huyo aliwapongeza walimu na uongozi mzima wa shule hiyo kwa kuwaandaa vema vijana katika sanaa za maonyesho walizoonyesha jukwaani lakini zaidi aliwamwagia sifa kwa mwaka huu kushika nafasi ya pili kiwilaya katika mitihani ya moko darasa la saba wa halmashauri ya Chalinze na ule wa mkoa wa Pwani.


"Mwaka 2021 mlipata mtoto aliyekwenda kipaji katika sekondari ya Mzumbe. Niwatake na mwaka huu mfanye hivyo zaidi ili kuonyesha ubora wenu katika taaluma.


Akimkaribisha mgeni rasmi kuongea mwalimu mkuu wa shule hiyo Mtawa-Robson Mathew alisema mwaka huu kuna wahitimu 45 wa darasa la saba, wavulana 22 na wasichana 23 wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa Taifa mapema mwezi ujao.


Mahafali hiyo ilihudhuriwa pia na Afisa elimu kata ya Bwilingu Mwl. Denis Joseph, Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw. John Kirumbi, Meneja wa shule Mtawa-Merry Josmel, baadhi ya wakuu wa shule katika halmashauri ya Chalinze pamoja na wazazi wa wanafunzi wa jumuiya ya shule hiyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post