KINACHOENDELEA FAINALI LIGI YA DR. SAMIA - KATAMBI CUP

 

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MASHINDANO ya ligi ya Dr.Samia/ Katambi yanatamatika leo katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) kati ya timu ya Masekelo na Ngokolo.

Fainali hiyo inachezwa leo Agosti 31,2024 huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa.

Kabla ya mchezo huo wa fainali, ulitanguliwa na mchezo wa awali ilikutafuta mshindi wa tatu kati ya timu ya Kashwasa na Kolondoto, ambapo Kashwasa waliibuka na ushindi kwa kupata magoli mawili, na hivyo kuwa washindi wa tatu ambao wataibuka na kitita cha Sh.milioni Moja.
Mgeni Rasmi mwenyekiti wa CCM Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa fainali hiyo, amempongeza Mbunge Katambi, kwamba amemuheshimisha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia jina lake kwenye mashindano hayo na pia Rais ni mpenda michezo na amemuunga mkono kwa vitendo.

Amesema ligi hiyo imeibua vipaji vingi vya vijana na watapata ajira kupitia ligi hiyo, sababu mchezo kwa sasa ni ajira na vijana wengi wamepata ajira kupitia michezo.
Aidha, katika mashindano hayo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha Sh.milioni 6, wa pili milioni 3 na watatu milioni Moja, huku mshindi wa kwanza akiibuka pia na kombe pamoja na mfugaji bora akiibuka na kiatu na goli kipa bora na pia zawadi kemkem zitatolewa ikiwamo mipira.

Endelea kufuatilia mtandao huu kwa taarifa zaidi hapo baadae….

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post