WATOTO YATIMA WAPATIWA HUDUMA ZA ELIMU BORA NA SHIRIKA LA MASISTER




Mwandishi wetu,Moshi,

Watoto yatima na waishio katika mazingira magumu kutoka maeneo mbalimbali wamepatiwa huduma za elimu bora na shirika la masister wa shirika damu takatifu ya Yesu,ikiwa ni moja sehemu ya huduma yako.

 
Akizungumza na wandishi wa habari msimamizi wa kituo cha watoto yatima Upendo-OKAT iliyopo Njia Panda wilaya Moshi mkoani Kilimanjaro,Sister Deodora Mtagona kutoka shirika la damu takatifu ya Yesu,ameeleza namna ambavyo waliweza kuwasaidia watoto hao.


Sister Mtagona amesema watoto yatima na waishio katika mazingira magumu wameweza kupatia elimu pamoja na huduma za kiroho na kimwili,huko wakifanyiwa ushauri nasa ili waweze kufikia ndoto zao za maisha.


Amesema kuwa chimbuko la kituo hicho ni kutokana na watoto yatima na wale wamazingira magumu kukosa huduma muhimu ikiwemo elimu,afya na malazi.

Amesema kituo hicho kinajiendesha kwa nguvu za wadau mbalimbali ikiwemo mama Rioba Mosha mhadhiri chuo kikuu cha marekani baada ya kuja Tanzania na wanafunzi wake kuguswa na adha na maisha magumu ya watoto yatima.

Aidha amesema mama Rioba Mosha aliona na kuguswa kuwasaida vijana wakitanzania ili waweze kufikia ndoto zao.


"Mwaka 2020 mama Rioba Mosha mhadhiri chuo kikuu cha marekani alikua Tanzania na kutembelea kituo cha watoto yatima cha Upendo children home iliyopo shanty na kupewa historia ya kituo ambapo kinalea watoto wachanga na baada ya  kufikia umri wa miaka ya mitano nakuhamishwa kwenda maeneo mbalimbali,ndiyo alianzisha bodi Tanzania na marekeni ndipo kikajengwa hiki kituo,"amesema.


Amesema kuwa kituo hicho kwa sasa kinawatoto wa 26,kati ya hao wakiume 11 wakike 15 na kwamba watoto wote wanasoma.

"Baadhi yao wako shule ya sekondari na msingi ambapo wanasoma katika shule mbalimbali za binafsi,asubuhi wanapelekwa shule na jioni wanarudishwa kulala kituoni,".

Katika hatua nyingine sister Mtagona ametoa wito kwa jamii kuonyesha upendo kwa watoto na kuwalea katika mazingira bora bila kuwatelekeza.

Amesema watoto ni baraka kutoka kwa Mungu hivyo hatua budi kuwapenda na kuna kuwajali.

 Kwa upande wake mjumbe wa Bodi ya kituo hicho Antony Semagi amesema kuwa bodi hiyo imeona umuhimu wakuwaendeleza watoto hao ili waweze kujitegemea.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post