WANAHARAKATI WASHAURI ELIMU ITOLEWE KWENYE USHIRIKI WA KUTOA MAONI KATIKA NGAZI ZA UAMUZI


WADAU wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS),wameshauri utoaji wa elimu kwenye jamii kuhusiana na umuhimu wa ushiriki wa kila mtu kwenye kutoa maoni katika ngazi za maamuzi kuanzia nyumbani hadi kufikia kwenye serikali kuu.

Akizungumza leo Julai 17,2024 Jijjini Dar es salaam,katika viunga vya ofisi ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Mwanaharakati wa masuala ya Jinsia, Slivia Sostenes amesema jamii inatakiwa ielewe umuhimu wa ushiriki katika mgawanyo wa mali na rasilimali kuanzia ngazi ya familia kabla ya kufikia katika ngazi ya Taifa.

Aidha Slivia ameeleza kuwa wametambua muhimu kwa kila mtu kutoa maoni yake hasa kwenye vikao vinavyoanzia katika ngazi ya mtaa hadi ngazi za juu.

"Kuna umuhimu mkubwa kwa kila mmooja kuchangia mawazo yake kwenye uongozi,kukosoa na kupongeza pale inapotakiwa" Slivia ameeleza.

Pamoja na hayo Slivia amegusia suala la mgawanyo sawa wa mali na rasilimali ambapo amesema ni muhimu kila kundi likahusishwa bila kuacha kundi lolote kuanzia ngazi za chini kabisa kwenye familia hadi serikali kuu.

Kwa upande wake, Mwanaharakati wa Jinsia Cesilia Michael ameiomba serikali kuhusisha wananchi katika mipango yao kwa lengo la kuhakikisha huduma wanazozitoa zinakidhi mahitaji jamii.

Nae, Mdau wa Semina za Jinsia kata ya Manzese, Wilaya ya Ubungo, Kennedy Anjelita amesema rasilimali zinazotengwa na serikali haziwanufaishi walengwa moja kwa moja kutokana na uongozi kuwanufaisha watu wao wa karibu.

"Serikali lengo lao kila mtu anufaike lakini mchakato wa maandalizi hadi kufikia hatua ya mwisho hauko sawa,kutokana na baadhi ya viongozi ambao wanasimamia hizo rasilimali kutokuwa na usawa wakijinsia"amesema.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post