VIJANA WASHAURIWA KUPIMA VVU KUKABILIANA ONGEZEKO LA MAAMBUKIZI YA VVU 
Na Christina Haule, Morogoro 

MWAKILISHI wa Mtandao wa vijana wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Tanzania Cyprian Komba amewataka vijana kujitokeza kupima  Virusi vya UKIMWI ili kukabiliana na ongezeko la maambukizi linalowakumba vijana.
Kwa mujibu wa utafiti wa viashiria vya UKIMWI uliofanywa na Serikali mwaka 2022/23 watu 60,000 wamepata maambukizi ya VVU huku asilimia 40 ya maambukizi hayo ni kutoka kwenye kundi la vijana wa miaka 15-24.

Komba alisema hayo kwenye kongamano la vijana juu ya elimu ya masuala ya UKIMWI lolilofanyika kwenye chuo kikuu cha SUA mkoani hapa.

Alisema katika asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi hayo mwaka 2022/23 asilimia 80 ni vijana wa kike.

Komba alisema Serikali imehakikisha inaweka sehemu ya vijana kwenye kutoa maamuzi ili kueleza mapendekezo yao juu ya VVU na walipo sababu mwanzoni vijana hawakupewa nafasi.

Alisema takwimu za mwaka 2022 za utafiti wa DHIS zinasema bado uelewa wa vijana kwenye masuala ya VVU upo chini na kufanya Serikali kushirikiana na Asasi mbalimbali za kiraia kuwaelimisha kupitia makongamano ili wapime na kujua afya zao .

Naye mmoja wa wanafunzi wa SUA Nora Charles aliishukuru NACOPHA kwa kuwapatia elimu hiyo itakayowafanya kuzingatia afya zao kwa kupima kwa ajili ya kuimarisha afya zao na kufikia malengo waliyokusudia.

“tumeanza kupata uelewa kuwa tusipopima hatutotimiza ndoto zetu na kubaki na miili dhoofu ikiwa tuna maambukizi bila kujua na tukipima hata kama tukikutwa na maambukizi bado tunayonafasi ya kutimizia malengo yetu kwa kupata na kuanza kutumia dawa za kufubaza makali ya UKIMWI (ARV)” Alisem.a

Awali Mwakilishi wa TACAIDS Charles Hinju aliwaasa vijana kujiepusha na hali hatarishi za kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa kuacha kuiga Maisha ya wengine na kuzimudu hali za miili yao.

Alisema mtu anakuwa hatarini kupata maambukizi kutokana na kutofanyiwa tohara, unyanyasaji wa kijinsia, umaskini wa kipato unaopatikana kutokuwa na kuishiwa fedha za matumizi ‘boom’ na hivyo kutafuta wa kuwasaidia na kuangukia kwenye magonjwa. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post