RC MWASA AWAASA WAUMINI KUJIEPUSHA NA UKATILI

Na Mwandishi wetu, Kagera

Mkuu wa Mkoa wa  Kagera Mhe Hajat Fatma Mwassa amewaomba Viongozi wa madhehebu ya Dini kuendelea kuwalea kimaadili waumini wao jambo ambalo litasaidia  kuepukana na Vitendo ĺvya Kikatili.

Bi. Hajat Mwassa ametoa wito huo  wakati wa Ibada ya Shukrani ya Uchungaji pamoja na  Maombezi Maalum ya Kuliombea Taifa na Viongozi, iliyofanyika katika Viwanja vya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Lweru Wilayani Muleba mapema Julai 28, 2024 wakati alipoambatana na Mgeni Rasmi Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa kwa niaba ya Waziri Mkuu.

 *"...Katika Mkoa wetu wa Kagera kuna mshikamano mkubwa wa viongozi wa Dini zote na leo hii mshikamano huo unaonekana  mahala hapa, Baba Askofu Mbelwa kawaalika Viongozi wa Dini nyingine na kuungana naye ili kumwombea Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na wasaidizi wake kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa misingi ya haki, Utawala bora, hekima na busara...* 

 *Tunapowaombea Viongozi wetu wa Kitaifa na kuliombea amani na utulivu Taifa letu la Tanzania nitumie fursa hii pia kuwakumbusha ninyi Viongozi wetu wa Dini kuendelea kukemea vikali vitendo vya kikatili katika jamii zetu hususani ukatili kwa watoto. Niwaombe muendelee kuwahubiri waamini wetu katika nyumba zetu mbalimbali za ibada Wananchi kutojihusisha na vitendo hivyo vya ukatili kwa binadamu wenzetu..."* Amesema Hajat Mwassa 

Ibada hiyo imeambatana na Harambee ya Ujenzi wa Makao Makuu ya Kanisa hilo Mkoani Kagera ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imechangia shilingi Milioni Moja.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post