MHANDISI MKAMA BWIRE, KAIMU AFISA MTENDAJI MKUU DAWASA

 

Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika tarehe 03 Julai, 2024 ofisi za DAWASA Dar Es Salaam.


Mhandisi Bwire ni Mtumishi wa Wizara ya Maji ambae amehudumu kama Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Kibaha, Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Tabora (TUWASA) na hadi anapokea jukumu hili alikuwa ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini katika Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post