DAWASA NDANI YA KISARAWE KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI AWESO

 


Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetekeleza agizo la Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) la kufika na kukutana na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Magoti kwa ajili ya kutatua changamoto ya huduma ya maji katika wilaya hiyo.

Akizungumzia mipango iliyopo ya Mamlaka, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire ameeleza katika kutatua changamoto ya huduma ya maji wilaya Kisarawe imeandaa mpango wa muda mfupi na mrefu ili kuanza kazi mara moja ya kuwahudumia wananchi.

Amebainisha kuwa katika Kata ya Kiluvya tayari Mamlaka kwa kushirikiana na Wakala wa maji vijijini (RUWASA) kutalazwa miundombinu ya usambazaji maji katika tenki la maji la RUWASA lenye ukubwa wa lita elfu tisini na kuyasambaza kupitia vizimba 4 vilivyopo katika hatua ya awali.

"Baada ya maboresho hayo mtaa wa Makurunge maeneo ya Mwanakondoo, Majumba sita, Kwa masista, Relini, Mji mpya, Bi. semeni na Bi. ngoma" alisema Mha. Bwire.

"Hatua ya pili sasa tutafanya usanifu wa mradi mzima ambao ndio utakao kuwa wa muda mrefu ambapo utajumuisha na mradi wa matenki ya maji ya NSSF waliokabidhi ilikusaidia kuhudumia katika kata Kiluvya" alisema Mha. Bwire

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Petro Magoti ameipongeza serikali kupitia DAWASA kwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo ambapo ameeleza huduma ya maji ni fursa ya kufungua kiuchumi wilaya ya Kisarawe kupitia uanzishwaji wa viwanda vinavyotegemea huduma hiyo katika eneo lilotengwa kwa ajili ya viwanda.

"Sisi tutashirikiana kama timu moja kuanzia ofisi yangu hadi diwani, nia yetu ni Kisarawe isonge mbele kwa maendeleo maana mimi ni DC wa kimataifa" alisema Mhe. Magoti

Naye Diwani wa kata ya Kiluvya Mhe. Aidan Kitile amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi wa Mamlaka ikiwemo katika kufanyia kazi kero zinapo ripotiwa na wananchi kwa wakati maslani uvujaji wa maji.

"Mamlaka ni vyema muwe mnawapa watumishi wenu mafunzo ya mara kwa mara itasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma zenu" alisema Mhe. Kitile.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post