TPDC YATOA BILIONI MOJA UJENZI WA VITUO VYA AFYA, MTWARA


Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma za kijamii kwenye maeneo ambayo shughuli za utafutaji, uzalishaji, usafirishaji na usambazaji wa gesi aislia zinafanyika.

Huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo afya, elimu, maji na utawala bora zinaimarishwa ikiwa ni sehemu ya Uwajibikaji wa Shirika kwa Jamii (CSR). 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa TPDC  Marie Msellemu amesema Shirika hilo  limetoa jumla ya Bilioni moja ili kuinua sekta ya afya mkoani Mtwara ambapo milioni 600 zimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya  kijiji cha Msimbati na Tsh milioni 400 zimetolewa kukamilisha ujenzi wa kituo cha afya kijiji cha Nyundo  kilichopo Kata  ya Nyundo wilaya ya Nanyamba. 
Aidha, akiongea na wananchi wa Nanyamba, Mbunge wa Nanyamba Chikota ameishukuru TPDC kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali kwenye kuboresha sekta ya afya. 

"TPDC amekuwa mdau wetu mkubwa wa maendeleo mkoano Mtwara, tunashukuru uongozi wa TPDC kwa kutupa fedha za kukamilisha kituo cha afya kata ya Nyundo Tsh milioni 400 ambapo kukamilika kwa kituo hiki cha afya tunatarajia  kitawapunguzia wananchi gharama za usafiri ili kufuata huduma", alieleza Chikota. 

Wananchi wa kijiji cha Nyundo  wameishukuru TPDC   kwa kutoa fedha za kamilishakutoa ujenzi wa Zahanati hali ambayo itapunguza vifo hasa vya kina mama wajawazito.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post