SHEIKH KABEKE AZINDUA MASHINDANO YA MUFT ABUBAKAR ZUBERI

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Hassan Kabeke amezindua Mashindano ya Muft Abubakar Zuberi yaliyoanza kutimua vumbi leo katika Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza. 

Mchezo huo wa ufunguzi unawakutanisha timu ya Viongozi wa BAKWATA Mkoa wa Mwanza ambao wanachuana na timu ya Kamati ya Amani Mkoa wa Mwanza. 

Akizindua Mashindano hayo Sheikh Kabeke ameitaka jamii kudumisha Amani na utulivu  nchini huku akiwaasa waumini wa dini mbalimbali kutenda yaliyo mema kwa mujibu wa mafundisho ya dini. 

Pia Sheikh Kabeke ameitaka jamii kujiepusha na Imani za kishirikina ambazo zimekuwa zikisababisha mauaji dhidi ya watu wenyewe ulemavu wa ngozi (Albino)

"Vitendo vya ukatili na mauaji ni kinyume na mafundisho ya Mwenyezi Mungu hivyo ni wajibu kwetu sote kuvikemea" ,amesema Sheikh Kabeke. 

Fainali ya Mashindano hayo yanayoshirikisha timu nane inatarajia kufanyika Jumapili ya Julai 7, 2024 ambapo mshindi atajinyakulia ng'ombe mnyama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post