AUSTRALIA NA AFRIKA MASHARIKI WAIMARISHA UHUSIANO KUPITIA KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI LA SOKA

Mchezaji wa Taifa Stars na klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine, Novatus Dismas, akizungumza na vijana kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wakati wa uzinduzi wa mashindano ya East Africa Cup hivi karibuni katika viwanja vya Moshi Tech, jijini Moshi mkoani Kilimanjaro. Mashindano hayo yaliandaliwa chini ya udhamini wa Ubalozi wa Australia na UNESCO kwa lengo la kukuza uwezo wa vijana waweze kuwa mawakala wa kuleta mabadiliko Chanya ndani ya jamii zao na kukuza ushirikiano baina ya vijana kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki. Picha: Mpiga Picha wetu.

Australia imeendelea kukuza mahusiano ya karibu na nchi za mashariki mwa Afrika kupitia tukio la wiki hii la mashindano ya kombe la Afrika Mashariki (East Africa Cup) – mashindano yanayofanyika kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha michezo kama nyenzo ya kuwawezesha vijana. 

Mchango endelevu wa Australia katika kombe hilo umechangia ongezeko la ushiriki wa mabinti Pamoja na kuvuta uwakilishi zaidi kutoka mataifa mbalimbali katika ukanda huu.

Mashindano ya kombe hilo yanafanyika wiki hii mjini Moshi, Tanzania ambapo vijana watashiriki kwenye michuano ya mpira wa kikapu (basketball), mpira wa miguu na chess Pamoja na kushiriki kwenye karakana zinazolenga kuimarisha amani, uraia na uhusiano wa kijamii.

Mchezaji mpira mkongwe, Novatus Dismas ambae kwasasa anachezea klabu ya Shakhtar Donetsk ya nchini Ukraine ambayo inashiriki michuano ya mabingwa wa ulaya UEFA anatarajiwa kuungana na mwamuzi wa FIFA kutoka Tanzania, Ahmed Arajiga kuzindua rasmi hafla ya mashindano hayo, Juni 20, 2023.

Wachezaji wenye uraia mchanganyiko wa ukanda wa Afrika mashariki na taifa la Australia wamekuwa wakifanikiwa sana kwenye mpira wa miguu ambapo Nestory Irankunda, mchezaji wa Australia mwenye asili ya Tanzania ambae anaiwakilisha timu ya taifa ya wanaume ya Australia na kujiunga na klabu ya Bayern Munich, mwezi Julai 2024. Mwanasoka mwenza kutoka Australia mwenye asili ya Kenya, Awer Mabil, ambae hivi sasa anaichezea timu ya taifa ya Australia pamoja na Klabu ya Grasshoppers inayoshiriki michuano ya Swiss Super League club.

Akizungumzia mashindano hayo, balozi wa Australia nchini Kenya, Jenny Da Rin, amesema: “Australia inajivunia kuunga mkono mashindano ya Kombe la Afrika Mashariki ili kusaidia kuwezesha, kuhamasisha na kukujuza ujuzi wa vijana wa Afrika Mashariki kupitia michezo.

“Mchezo wa Soka nchini Australia umekuwa ukikua kwa kasi sana. Mwezi Julai 2023, Australia ilikuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia la wanawake na inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano ya wanawake la kombe la bara la Asia ya AFC. Tunajivunia kuona namna wachezaji wa Australia wenye asili ya Afrika Mashariki wanavyofanya vizuri duniani na nchini Australia, jambo linalowahamasisha wanamichezo wapya. Tunatarajia kuona zaidi wanamichezo kutoka Afrika Mashariki wakichezea timu zetu za taifa na katika viwango vya juu katika michuano ijayo ya kombe la dunia,” alisema.

Kwa upande wake, Elly Goro, Mratibu wa Kombe la Afrika Mashariki (East Africa Cup) alisema kuwa michuano hiyo ni zaidi ya mashindano ya soka, akibainisha kuwa kumekuwa na ushirikiano wa karibu na washirika ili kusaidia kukuza uwezo wa vijana waweze kuwa mawakala wa kuleta mabadiliko Chanya ndani ya jamii zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post