ZAIDI YA BILIONI 8 ZIMETUMIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATA NSHAMBYA



Wajumbe wa mkutano mkuu wa Kata ya Nshambya wakitembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule yaSekondari Omumwani
Majengo ya Madarasa yanayojengwa katika kata ya Nshambya
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi kata ya Nshambya wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo Godson Gipson ambaye pia ni mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata hiyo
Diwani wa kata ya Nshambya (Aliyevaa Tishert ya Kijani) pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi kata ya Nshambya wakisikiliza taarifa ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali yakiwemo madarasa  pamoja na Mabweni katika Shule ya Sekondari Omumwani ambayo imesomwa na mwakilishi wa mkuu wa shule hiyo
Diwani wa Kata ya Nshambya Godson Gipson akiwa na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini pamoja na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Nshambya wakati wa kutembelea miradi ya Maendeleo

Na Mariam Kagenda _Kagera


Zaidi ya shilingi bilioni 8 zimetumika katika   utekelezaji wa miradi mbalimbali ya  maendeleo   kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba  mkoani Kagera jambo ambalo limepelekea changamoto nyingi za wananchi kutatuliwa kutokana na miradi iliyojengwa hasa wanafunzi kusomea katika mazingira mazuri.

Diwani wa kata ya Nshambya Bwana Godson Gipson amesema hayo baada ya ziara  ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi kata ya Nshambya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya Maendeleo katika kata hiyo .

Bwana Gipson amesema kuwa ipo miradi mingi ya maendeleo ambayo imetekelezwa katika kata hiyo tangu mwaka 2020_2024 na mingine utekelezajii wake unaendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya nadarasa, matundu ya vyoo katika shule za msingi na Sekondari, ujenzi wa Mabweni ,Ujenzi wa  majengo mbalimbali katika hospital ya wilaya  iliyopo katika kata hiyo.


Ameongeza kuwa Kata hiyo imepata Printer , Computer katika shule ya Sekondari Nshambya , madawati,Meza ambapo fedha hiyo imetolewa na serikali pamoja na wafadhiri jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa  kupunguza changamoto kwa wananchi wa kata hiyo kutokana na utekekezwaji wa miradi hiyo.

Amesema kuwa miradi hiyo isingeweza kutekelezwa kama hamna ushirikiano wa kutosha kwa viongozi waliopo  hivyo ushirikiano walionao kuanzia kwa Mbunge wa Jimbo hilo Adv Stephen Byabato, Madiwani pamoja na viongozi wengine wa kata hiyo umepelekea miradi hiyo kutekelezwa na mingine utekelezaji wake unaendelea .



Wakati wajumbe wa mkutano mkuu wa kata wa chama cha Mapinduzi kata ya Nshambya wakitembelea na kukagua miradi iliyotekelezwa wamesema kuwa wanaishukuru serikali chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan  kwa namna anavyoikumbuka kata hiyo kupitia kwa Mheshimiwa Mbunge pamoja na diwani na kuleta fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo .

Kwa upande wake Mwenezi wa Manispaa ya Bukoba Bwana Yazid Isaka amewaomba wajumbe hao kuendelea kutoa ushirikiano kwa viongozi waliopo madarakani ili waweze kuwa na nguvu ya kuendelea kuwatumikia hasa katika kutatua changamoto za wananchi .

Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na wajumbe hao ni pamoja na Ujenzi wa matundu 20 ya vyoo Katika shule ya msingi Nshambya ,Ujenzi wa vyumba vya madarasa ,ukamilishaji wa Maboma  na ukamilishaji wa Maabara ya Chemistry , ukarabati wa chumba cha Computer katika shule ya Sekondari Nshambya ,Shule mpya ya Nshamba B pamoja na daraja la Kyebitembe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post